Breaking News

Your Ad Spot

Mar 26, 2016

MOROCCO YAKAMATA MAGAIDI WALIOPANGA MASHAMBULIZI

Morocco yakamata magaidi waliopanga mashambulizi
serikali ya Morocco imetangaza kuwanasa kwa akali watu tisa kwa kuwa na mahusiano na kundi la kigaidi na kitakfiri la Daesh nchini humo.
Taarifa iliyotolewa jana na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Morocco imesema kuwa, watuhumiwa hao walitiwa mbaroni na polisi katika mji wa Marrakesh na miji mingine ya nchi hiyo wakati walipokuwa wakipanga shambulio la kigaidi. Katika ripoti hiyo, magaidi hao walikuwa wanakusudia kwenda Libya kwa ajili ya kujifunza mafunzo ya kijeshi. Wizara ya Mambo ya Ndani ya Morocco imetangaza kuwa, tangu mwaka 2013 hadi hivi sasa, imeshasambaratisha zaidi ya makundi 30 ya kigaidi nchini humo. Aidha katika kipindi hicho polisi wa nchi hiyo imevunja njama mbalimbali za kuharibu usalama na amani nchini. Ni vyema kuashiria hapa kwamba, asilimia kubwa ya wanachama wa kundi la kigaidi na kitakfiri la Daesh ni vijana kutoka Tunisi na Morocco.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages