Mwenyekiti
wa Tume ya Kurekebisha Sheria Jaji Aloysius Mujulizi (Kushoto)
akizungumza wakati wa kuwasilisha taarifa ya utafiti wa marekebisho ya
Sheria ya Manunuzi ya Umma, katikati ni Waziri wa Katiba na Sheria Mhe.
Dkt.Harrison Mwakyembe na kulia ni katibu Mkuu wa Wizara hiyo Prof.
Sifuni Mchome. Waziri
wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt.Harrison Mwakyembe akipokea taarifa ya
utafiti wa marekebisho ya Sheria ya Manunuzi ya Umma kutoka kwa
Mwenyekiti wa Tume ya Kurekebisha Sheria Jaji Aloysius Mujulizi.
Waziri
wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt.Harrison Mwakyembe akizungumza mara baada
ya kupokea taarifa ya utafiti wa marekebisho ya Sheria ya Manunuzi ya
Umma kushoto ni Mwenyekiti wa Tume ya Kurekebisha Sheria Jaji Aloysius
Mujulizi na kulia ni katibu Mkuu wa Wizara hiyo Prof Sifuni Mchome.
Picha zote na Raymond Mushumbusi MAELEZO
………………………………………………………………………………………
Na Jacquiline Mrisho -MAELEZO
Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt.Harrison
Mwakyembe amepokea taarifa ya utafiti wa marekebisho ya Sheria ya
Manunuzi ya Umma kutoka Tume ya kurekebisha Sheria.
Akipokea taarifa hiyo leo Jijini Dar es
salaam Mhe. Dkt.Harrison Mwakyembe amesema taarifa hiyo ya utafiti
itasaidia kurekebisha sheria ya manunuzi ambayo inalenga kukuza uchumi
wa nchi.
“Mimi na wataalamu wangu tumeipokea taarifa
hii, tutaiangalia na kuhakikisha tunaifikisha Wizara ya Fedha na Mipango
na kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali ili kuendelea na utaratibu
unaofuata ili mchakato wa marekebisho uweze kufanyika kwa haraka”alisema
Dkt Mwakyembe.
Akifafanua juu ya sheria ya manunuzi ya
Umma, Mwenyekiti wa Tume ya Kurekebisha Sheria Jaji Aloysius Mujulizi
amesema kuwa Tume imefanya utafiti wa sheria hiyo kwa kushirikisha wadau
mbalimbali.
“Tumepata maoni mengi na ushirikiano mkubwa
kutoka kwa viongozi na wasimamizi wa manunuzi ya Serikali kwa namna
wanavyoiona sheria ya manunuzi ya Umma,na sisi tumeyachambua maoni hayo
kwa kutumia vigezo vya sheria”alisema Jaji Mujulizi.
Aidha,Tume imetoa maoni kwa Serikali
kusimamia sheria ili iweze kuendana na ukuaji wa uchumi nchini kwa
kurekebisha baadhi ya sheria ili kuepuka muingiliano uliopo kati ya
sheria ya manunuzi na sheria nyingine.
Marekebisho ya sheria hii ni moja ya agizo
la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. John Pombe Magufuli
lililotolewa Novemba 2015 alipokua akizindua Bunge la 11.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269