Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Ally Mwalimu akiwa katika Mkutano wa 60 wa Kamisheni ya Umoja wa Mataifa kuhusu Hali ya Wanawake ( CSW). Kushoto kwake ni Mwakilishi wa Tanzania wa Kudumu Katika Umoja wa Mataifa, Balozi Tuvako Manong.
Na Mwandishi Maalum, New York
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Ally Mwalimu ( Mb) ametoa hutuba kwa niaba ya Kundi la Nchi za Afrika wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa 60 wa Kamisheni ya Umoja wa Mataifa kuhusu Hali ya Wanawake ( CSW).
Mkutano huu wa wiki mbili unawakusanya wawakilishi kutoka serikali mbalimbali duniani na Asasi za Kiraia ambapo hujadiliana na kubalishana uzoefu na kuelimishana kuhusu hatua mbalimbali ambazo serikali zao zinachukua katika kuboresha maisha ya mwanamke na mtoto wa kike.
Wakati
mamia ya wanawake kutoka serikalini na Asasi za Kiraia wakiwa
wanakutana hapa Umoja wa Mataifa kwa mkutano wao unaojadili hali yao
katika maeneo mbalimbali. Mamia mengine ya wanawake hususani wale wa
Afrika wanaendelea kukumbana na changamoto lukuki zinazowarudisha nyuma
kimaendeleo.
Ni
wanawake hao wanaoishi katika nchi zenye migogoro, vita visivyokwisha,
wenye kukabiliwa na uhaba na ukosefu mkubwa wa chakula, maji safi na
salama, matatizo yatokanayo na mabadiliko ya tabia nchi, ndio ambao
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Wazee, Jinsia na Watoto, Mhe. Ummy
Ally Mwalimu(Mb) ameitaka jumuiya ya kimataifa kuongeza kasi ya
ushirikiano ili malengo mapya ya maendeleo endelevu (Agenda 2030)
yaweze kuwafikia.
Waziri
Mwalimu ametoa wito huo jana jumatatu, wakati alipotoa hutuba kwa
niaba ya nchi za Afrika katika siku ya kwanza ya Mkutano wa 60 wa
Kamisheni ya Umoja wa Mataifa kuhusu Hali ya wanawake (CSW) ambao
umeanza hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa.
Changamoto
hizo pamoja na nyinginezo nyingi zikiwamo kutopata fursa ya huduma za
afya ya uzazi salama, elimu na usawa wa kijinsia zinamfanya mwanamke wa
Afrika ashindwe kushindana na wanawake wenzie hususani wale walioko
katika mataifa yaliyoendelea.
Waziri
Mwalimu ambaye anaongoza ujumbe wa Tanzania katika Mkutano huu wa wiki
mbili, alitoa hotuba hiyo kwa niaba ya nchi za Afrika kutokana na
kwamba Tanzania kupitia Uwakilishi wake wa Kudumu wa Tanzania katika
Umoja wa Mataifa ni Mwenyekiti wa Kundi la Nchi za Afrika kwa mwezi huu
wa March.
Amewaeleza
washiriki wa mkutano huo waliofurika katika Ukumbi Mkuu wa Mikutano wa
Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, kwamba ingawa pamekuwapo na makubaliano
na mapendekezo mengi kuanzia yale yaliyofikiwa huko Beijing, bado
mwanamke anayeishi katika nchi zenye migogoro na vita barani Afrika
ataendelea kuachwa nyuma na hivyo kukosa fursa ya kushinda na wenzie.
“
Ingawa vita, ukame wa kutisha, ukosefu wa chakula, ukosefu wa maji
safi, ukichanganya na ukosefu wa fursa za kiuchumi, kijamii na
kisiasa ni matatizo yanayowakabili watu maskini lakini mwanamke ndiye
anayeathirika zaidi,” alieleza Waziri Mwalimu.
Na
kuongeza kwamba Afrika inaendelea kutilia mkazo hoja ya
kuwashirikisha wanawake katika majadiliano na utoaji wa maamuzi katika
masuala yanayowagusa yakiwamo masuala yanayohusu mabadiliano ya tabia
nchi na usuluhishi wa migogoro.
Alieleza
kwamba, nchi zinazoendelea na zilizoendelea zinapashwa kuongeza
kasi ya ushirikiano na ubia baina yao ili kufanikisha utekelezaji wa
Agenda 2030), Makubaliano juu Mabadiliko ya Tabia nchi yaliyofikiwa
huko Paris Ufaransa mwaka jana na makubaliano yaliyofikiwa na
waafrika wenye kupitia Ajenda 2063 , ili katika umoja wake dunia basi
iweze kumwondoa mwanamke na jamii nzima kutoka hapa ilipo na kufikia
hali bora zaidi ya maisha.
Kama
hiyo haitoshi Waziri alisema, Afrika inaamini pia katika uwezeshwaji
wa Sekta binafsi, kupanua wigo wa ujasiliamali kama njia mojawapo ya
kukuza uchumi endelevu , usawa wa kijamii, usawa wa jinsia, ulinzi wa
mazingira na uwezeshaji wa mwanamke.
Mada
kuu ya Mkutano wa 60 wa Kamisheni ya Umoja wa Mataifa kuhusu Hali ya
Wanawake, ni “Uwezeshaji wa Wanawake na uhusiano wake na Ajenda 2030.
Awali
akizungumza mwanzoni mwa mkutano huu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa,
Ban Ki Moon amasema tangu alipoingia madarakani mwaka 2006 amejjitadi
kuongeza nafasi za viongozi wanawake katika Idara za Sekretarieti ya
Umoja wa Mataifa.
Akitilia
msisitizo hoja na haja ya kupanua wigo wa wanawake kushika nafasi
katika ngazi za juu za maamumizi, Ban Ki Moon amesema, ingawa nchi
nyingi zimejitahidi sana kuongeza ushiriki wa wanawake katika nafasi za
juu za uongozi bado kuna Nchi Tano ambazo hazina wanawake katika
Mabunge yao ili hali Nchi nyingine 7 hazina mawaziri wanawake katika
serikali zao.
Naye
Rais wa Baraza Kuu la 70 la Umoja wa Mataifa Bw Monges Lykketoft,
akizungumza wakati wa mkutano huo, pamoja na kusisitiza umuhimu wa
utekelezaji wa Agenda 2030 ambayo ameitaja kuwa ni jumuishi ameendelea
kupigia chapuo la kutaka Katibu Mkuu ajaye wa Umoja wa Mataifa awe
Mwanamke.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269