Breaking News

Your Ad Spot

Mar 19, 2016

NDEGE YA DUBAI YAANGUKA RUSSIA, 62 WAFARIKI

Ndege ya Dubai yaanguka Russia, 62 wafariki
Watu 62 wamefariki dunia mapema leo baada ya ndege ya abiria ya Shirika la Fly Dubai kuanguka wakati ikijaribu kutua katika mji wa Rostov-on-Don kusini mwa Russia karibu na mpaya wa nchi hiyo na Ukraine.
Ripoti zinasema kuwa ndege hiyo iliyotengenezwa Marekani aina ya Boeing738-800 ilianguka ikijaribu kutoa ikiwa imetoka Dubai nchini Imarati.
Msemaji wa Wizara ya Maafa nchini Russia Marina Kostioukova amethibitisha kutokea ajali hiyo lakini hakutoa maelezo zaidi. Abiria wote 55 na wahudumu 7 katika ndege hiyo wamepoteza maisha.
Shirika la Habari la RT limeripoti kuwa, uchunguzi wa awali umebaini kuwa ndege hiyo imeanguka kutokana na hali mbaya ya hewa katika uwanja huo wa ndege.Aghalabu ya abiria katika ndege hiyo ni raia wa Russia. Duru zinaarifu kuwa ndege hiyo ilijaribu kutua mara ya kwanza na kushindwa na kuanguka ilipojaribu kutua kwa mara ya pili.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages