Saudi Arabia na washirika wake wamezidisha mashambulizi ya anga dhidi ya makazi ya raia na maeneo ya ibada nchini Yemen.
Ripoti zinasema kuwa, ndege za kivita za Saudi Arabia na washirika
wake jana Alkhamisi zilifanya mashambulizi makubwa katika eneo la Sarwah
kwenye mkoa wa Maarib na kuua raia wengi. Mashambulizi hayo pia
yamesababisha hasara kubwa katika maeneo hayo. Ripoti zinasema kuwa
baadhi ya mashambulizi hayo yameua watu wote wa familia moja katika eneo
la al Qabitwa katika mkoa wa Lahaj.
Ndege za kivita za Saudia pia jana zilishambulia Msikiti wa al Wiraq
katika eneo la Misrakh na kuua Waislamu kadhaa waliokuwa ndani ya
msikiti huo.
Wakati huo huo Msemaji wa muungano unaopigana dhidi ya Saudia na
washirika wake huko Yemen amekadhibisha madai kuwa kumefikiwa mapatano
ya kusitisha vita baina ya wavamizi wa Kisaudia na harakati ya
Ansarullah na kusema watawala wa kifalme wa Riyadh wangali wanashambulia
maeneo mbalimbali ya Yemen na kumwaga damu za raia wasio na hatia.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269