Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Dkt.
Servacius Likwelile (kushoto) akiongea na waandishi wa habari leo jijini Dar es
salaam ambapo amesema kuwa wizara hiyo imeendelea kufanya vizuri katika ukusanyaji
wa mapato na katika kipindi cha mwezi Februari mwaka huu zimekusanywa zaidi ya Sh.
trilioni 1 tofauti na mwanzo ambapo zilikuwa zkikusanywa Sh.bil 850. Kulia ni
Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee, Mpoki
Ulusubisya.
Kamishna
Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Alphayo Kidata akifafanua kwa waandishi
wa habari leo jijini Dar es salaam jinsi Mamlaka hiyo ilivyofanikiwa kukusanya
mapato kutoka trilioni 1.2 kwa mwezi Disemba mpaka trilioni 1 na bilioni 79 kwa
mwezi Januari na kwa mwezi Februari wanatarajia kukusanya trilioni 1.013 na tayari
wamefikia nusu ya malengo waliyojiwekea.
Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi,Teknologia
na Mafunzo ya Ufundi Stadi, Maimuna Tarishi amesema Wizara yake itazitumia
fedha walizopewa mwezi huu kulingana na malengo yaliyokusudiwa ikiwemo fedha za
mafunzo kwa vitendo kwa wanafunzi wa Diploma na wanafunzi wa chuo kikuu. Wa
kwanza kushoto ni Kamishna Mkuu wa Mamlaka Tanzania (TRA) Alphayo Kidata
Katibu
Mkuu Wizara ya Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee
akifafanua namna Wizara yake ilivyojipanga kuzitumia fedha walizopata mwezi huu
ambapo amesema zitatumika kulingana na malengo yaliyokusudiwa ikiwemo fedha za mradi
wa ujenzi wa Chuo cha Tiba cha Kimataifa cha Muhimbili eneo la Mloganzila nje kidogo
ya jiji la Dar es Salaam.
Waandishi habari wakikusanaya taarifa
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269