Naibu
waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Dk. Hamisi
Kigwangalla amepongeza juhudi za Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA)
nchini kwa hatua wanazochukua katika utendaji wake ikiwemo zoezi la
kukagua madawa yasiyofaa kwa Jamii ikiwemo yale yaliyokwisha muda wake
hasa katika zoezi la "Operesheni Safisha" iliyofanywa karibu mikoa
mbalimbali ya Tanzania Bara huku akitaka wale wote waliohusika
kupandishwa Mahakamani kwa hatua za kushughulikiwa.
Kigwangalla
ameyasema hayo mapema jana Machi 17 jijini Dar es Salaam baada ya
kupewa matokeo ya Operesheni Safisha kwa maduka ya dawa muhimu na
yasiokuwa na vibali iliyofanywa na Baraza la Wafamasia na TFDA pamoja
na Jeshi la Polisi, amesema dawa zilizokamatwa zitaifishwe na kupeleka
katika hospitali za serikali.
Amesema
kuwa haiwezekani wananchi wakakosa dawa za serikali na kuonekana katika
maduka ya dawa na watu hao wakaachwa bila kuchukuliwa hatua.
Kigwangalla
amesema kuwa katika operesheni hiyo baadhi ya maduka yanauza dawa
ambazo haziko kwenye orodha za dawa ikiwemo ni dawa ya usingizi ambayo
inatakiwa kutumika wakati wa operesheni.
Aidha
amesema kuwa baadhi ya maduka mengine yamefungwa lakini yanauza dawa
nyakati za usiku na kuwataka wanaofanya operesheni kuendelea na
wataokutwa wachukuliwe hatua mara moja.
Operesheni
hiyo ilianza machi 1 hadi 3 mwaka huu ambapo walikagua maduka 685
katika mikoa tisa na kati hayo maduka 432 yamefungiwa kwa sababu
mbalimbali ikiwemo na kuwa na dawa za serikali pamoja na kuwa dawa za
asili.
Aidha
Kigwangalla amesema kuwa dawa ni sumu hivyo inatakiwa kutumika kwa
malengo yaliyokusudiwa na wanaouza dawa ambazo hawana orodha nazo
wanazalisha matatizo ya kiafya kwa wananchi
Kigwangalla
amesema hadi sasa ni dawa 65 tu ndiyo zenye nembo ya serikali na
kuwataka wananchi kutoa ushirikiano pale watakapopata dawa serikali
katika duka la dawa.
Amesema
kuwa jeshi la polisi lichukue hatua ya kuwabana wale wote waliokutwa
na dawa za serikali kuwabana katika kuweza kuwapata waliokuwa wakiwapa
dawa hizo.
Tazama MO tv, kuona tukio hilo hapa
Msajili wa Baraza la Famasi nchini, Bi. Elizabeth Shekalaghe akisoma
ripoti ya Operesheni Safisha kwa Naibu Waziri pamoja na wanahabari na
wakuu wa idara ya TFDA (hawapo pichani).
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA), Hiiti Sillo akitoa taarifa yake juuu ya Operesheni Safisha
Naibu
waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Dk. Hamisi
Kigwangalla akisoma tamko la Serikali ikiwemo juu ya kuwachukulia sheria
kali wahusika wanaohujumu sekta ya Afya hasa upande wa madawa tiba
ikiwemo watumishi wanaoiba dawa za Serikali pamoja na wale wanaoendesha
maduka ya dawa bila kuwa na vibari.
Baadhi ya maafisa kutoka TFDA na Famasia wakifuatilia tukio hilo.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Dk. Hamisi Kigwangalla akitoa tamko hilo.
Mwanahabari
wa mtandao wa Michuzi Blog, Bw. Chalila Chibuda akiuliza swali kwa
Naibu Waziri Dk. Kigwangalla (hayupo pichani) wakati wa tukio hilo.
Meza kuu ikisikilia swali kwa umakini kutoka wa wanahabari (hawapo pichani).
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Dk. Hamisi Kigwangalla akijibu maswali ya wanahabari.
Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Dk. Hamisi
Kigwangalla akiwaonesha wanahabari baadhi ya vitu vilivyokamatwa katika
Opresheni Safisha. kifaa alichokishika Naibu Waziri ni miongoni mwa
vifaa vilivyokutwa vinatumika kuchemshia vifaa vya kufanyia
upasuaji/operesheni ikiwemo vifaa vya kutolea mimba.
Baadhi ya vifaa na madawa vilivyokutwa wakati wa operesheni hiyo.
Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Dk. Hamisi
Kigwangalla moja ya dawa ambayo ni ya usingizi hata hivyo ilikutwa
katika maduka ya dawa ya kawaida
Madawa hayo.
Madawa hayo yaliyokamatwa.
Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Dk. Hamisi
Kigwangalla akitoa agizo la Kiserikali juu ya hatua zitakazochukuliwa
dhidi ya wahusika waliokamatwa kwa kukutwa na dawa zilizokwisha muda
wake, maduka yasiyokuwa na wafamasia waliosomea na yale yenye kuendeshwa
kienyeji.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269