Breaking News

Your Ad Spot

Mar 29, 2016

TAMASHA LA PASAKA LAHITIMISHWA MJINI KAHAMA

2
Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion Bw. Alex Msama akimpokea Mkurugenzi wa Utawala Wizara ya Ujenzi na Mawasiliano Bi. Katolina Kipa Mgeni rasmi wa Tamasha la Pasaka ambaye alimwakilisha Waziri wa Ujenzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa katika tamasha hilo lililofanyika kwenye uwanja wa Taifa mjini Kahama leo na kuhudhuriwa na Mkuu wa wilaya ya Kahama Mh. Vita Kawawa, Mbunge wa jimbo la Kahama Mh. Jumanne Kishimba na aliyewahi kuwa mbunge wa jimbo hilo Ndugu James Lembeli.
Waimbaji mbalimbali wametumbuiza katika tamasha hilo ambalo ndilo limehitimisha matamasha ya pasaka ya mwaka huu yaliyofanyika katika mikoa ya Geita , Mwanza na Shinyanga katika kanda ya ziwa, Waimbaji hao ni Upendo Nkone, Jennifer Mgendi, Boniface Mwaiteje, Martha Baraka, Goodluck Gozbert , Jesca BM, Christopher Mwahangila, Ephraim Sekereti na wengine wengi. (PICHA NA JOHN BUKUKU-FULLSHANGWE-KAHAMA)
4
Mkurugenzi wa Utawala Wizara ya Ujenzi na Mawasiliano Bi. Katolina Kipa Mgeni rasmi wa Tamasha la Pasaka ambaye alimwakilisha Waziri wa Ujenzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akizungumza na Mkuu wa wilaya ya Kahama Mh. Vita Kawawa Kushoto ni Mbunge wa jimbo la Kahama Mh. Jumanne Kishimba.
5
Mkurugenzi wa Msama Promotion Bw. Alex Msama akisalimiana na Bw. James Lembeli wakati alipokuwa akipmokea kwenye uwanja wa Taifa mjini Kahama leo.
1
Mwimbaji Tumsifu Rufutu akiimba huku akiwa amevalia kama manabii wa zamani wakati alipotumbuiza katika tamasha la Pasaka mjini Kahama leo.
6
Mwimbaji Jesca BM akifanya vitu vyake jukwaani.
8
Mshabiki wa muziki wa injili wa mjini Kahama Grace Boyo na rafiki yake Sara Shija wakifuatilia burudani ya muziki wa injili iliyokuwa ikiporomoshwa na waimbaji katika tamasha hilo.
9
Mwimbaji Faustine Munishi akisalimiana na Mkuu wa wilaya ya Kahama Mh. Vita Kawawa na viongozi wengine mara baada ya kuimba nyimbo zake mbili katika tamsha hilo.
10
Msabiki wa muziki wa injili wa mjini Kahama Grace Boyo na rafiki yake Sara Shija wakifuatilia burudani ya muziki wa injili iliyokuwa ikiporomoshwa na waimbaji katika tamasha hilo.
11
Mashabiki mbalimbali wa muziki wa injili wakipiga picha za Selfie katika tamasha hilo.
12 13
Mwimbaji Martha Baraka na wacheza shoo wake wakifanya vitu vyao jukwaani.
14
Tamasha hilo pia limehudhuriwa na watu mbali mbali kama unavyoona katika picha hii.
15
Mwimbaji Ephraim Sekereti akiimba nyimbo za kusifu na kuabudu katika tamasha hilo.
16
Mkurugenzi wa Msama Promotion akipiga picha ya pamoja na waimbaji wa kwaya ya Grorius ya Kahama mkoani Shinyanga.
17
Mwimbaji Boniface Mwaiteje akifanya vitu vyake jukwaani huku mashabiki wakicheza kwa furaha.
18
Mashabiki wakicheza kwa furaha katika tamasha hilo lililofanyika kwenye uwanja wa Taifa mjini Kahama.
19 20
Mkurugenzi wa Msama Promotion Bw. Alex Msama akicheza na wanakwaya wa Kwaya ya Grorius ya Kahama.
21
Mwimbaji Jeniffer Mgendi akiimba jukwaani.
22
Mwimbaji Goodluck Gozbert akipagawisha jukwaa katika tamasha hilo.
23
Mkurugenzi wa Utawala Wizara ya Ujenzi na Mawasiliano Bi. Katolina Kipa Mgeni rasmi wa Tamasha la Pasaka ambaye alimwakilisha Waziri wa Ujenzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akisoma hotuba kwa niaba ya waziri Profesa Mbarawa katika tamasha hilo kushoto ni Alex Msama wa pili kutoka kulia ni Mkuu wa wilaya ya Kahama Mh. Vita Kawawa na Mbunge wa jimbo la Kahama Mh. Jumanne Kishimba.
24
Mwimbaji Upendo Nkone akiwaimbisha mashabiki wake wakati alipokuwa akitumbuiza jukwaani kwenye uwanja wa Taifa mjini Kahama.
25
Mwimbaji Boniface Mwaiteje na Faustine Munishi kutoka nchini Kenya wakifanya mambo makubwa jukwaani kama wanavyoonekana.
26
Mwimbaji Faustine Munishi akionekana kufurahiswa na mashabiki wakati alipokuwa akiimba jukwaani kwa kushirikiana na mwimbaji Boniface Mwaiteje.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages