Breaking News

Your Ad Spot

Mar 3, 2016

UNESCO:IDADI YA WASICHANA MARA MBILI YA ILE YA WAVULANA HAWATOANZA SHULE KAMWE


 Takribani
wasichana milioni 16 wenye umri wa kati ya miaka 6 na 11 asilani hawatopata
fursa ya kusoma wala kuandika kwenye shule za msingi , ikilinganishwa na
wavulana milioni 8, iwapo hali ya sasa itaendelea, kwa mujibu wa ripoti kutoka
taasisi ya takwimu ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sanyansi na
Utamaduni( UNESCO )

Katika kuelekea siku ya kimataifa ya wanawake hapo Machi
8 takwimu hizo za UNESCO kuhusu "usawa wa kijinsia katika elimu"
zinaonyesha kwamba wasichana bado ni wa kwanza katika kunyimwa haki ya elimu
licha ya juhudi zote zilizofanyika na hatua zilizopigwa katika miaka 20
iliyopita.

Ripoti inasema pengo la kijinsia ni kubwa hasa katika
mataifa ya Kiarabu, Afrika Kusini mwa jangwa la Sahara na Kusini na Magharibi
mwa Asia.

Imeongeza kuwa Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara
wasichana milioni 9.5 hawatowahi kuhudhuria shule ikilinganishwa na wavulana
milioni 5.

Kwa jumla watoto zaidi ya milioni 30 wa umri wa miaka 6
hadi 11 hawasiomi.


Na pengo ni kubwa zaidi katika mataifa ya Kiarabu ambako
asilimi 80 ya wasichana hawasomi ikilinganishwa na asilimi 16 ya wavulana .

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages