WAZIRI MWAKYEMBE ATOA RAI KWA TAASISI MBALIMBALI NA WADAU KUIPITIA RIPOTI YA UCHAGUZI MKUU ULIOPITA ILI KUBORESHA CHAGUZI ZINAZOKUJA
Mgeni rasmi,Waziri wa sheria na Katiba Dkt Harrison Mwakyembe akifafanua
jambo mbele ya Wanahabari (hawapo pichani),kuhusiana na Ripoti ya maoni
ya jumla kuhusu uchaguzi Mkuu uliopita,aliyoipokea kutoka kwa
Waandaaji CEMOT (umoja wa taasisi za waangalizi wa ndani wa uchaguzi
inayohusisha Kamati ya Uangalizi wa Uchaguzi (Temco) na Muungano wa
taasisi zisizo za kiraia za kusimamia uchaguzi (Tacceo) ),kwenye semina
iliyofanyika leo katika ukumbi wa mikutano wa Hyatt Hotel jijini Dar na
kuwakutanisha Wadau mbalimbali wakiwemo Tume ya Uchaguzi
(NEC),Polisi,PCCB pamoja na Nchi Wahisani .Pichani kushoto ni Mjumbe wa
kamati ya CEMOT Bwa.Ezekiel Massanja
Katika mahojiano mafupi na Waandishi wa habari mara baada ya kuipokea
ripoti hiyo,Dkt Mwakyembe alisema kuwa Ripoti hiyo iliangalia mapungufu
yaliyokuwepo na namna ya kuyaboresha,Dkt Mwakyembe ametoa rai kwa
Serikali,taasisi mbalimbali na wadau wengine waweze kuipitia ripoti hiyo
na kujadiliana ili kuboresha chaguzi nyingine zinazokuja.
Wa pili kulia ni Mgeni rasmi,Waziri wa sheria na Katiba Dkt Harisson
Mwakyembe akiandika jambo wakati ripoti ya maoni ya jumla kuhusu
uchaguzi Mkuu uliopita,aliyoipokea kutoka kwa Waandaaji CEMOT
ikisomwa.
Mkuu wa Waandaaji wa Ripoti ya maoni ya jumla kuhusu uchaguzi Mkuu
uliopita (CEMOT),Dkt.Alexander Makulilo akisoma ripoti hiyo mbele ya
Wadau na walioshiriki kuiandaa ripoti hiyo.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269