Breaking News

Your Ad Spot

Apr 11, 2016

ANNE KILNGO MALECELA AFUTWA KAZI, IKULU YASIKITISHWA NA TAARIFA YA MAMA HUYO KUWA SHINYANGA HAKUNA MTUMISHI HEWA

MKUU wa mkoa wa Shinyanga, Anna Kilango Malecela (pichani),  amekuwa muhanga wa kwanza wa ngazi ya ukuu wa mkoa, kufukuzwa kazi mapema na Rais Dk. Magufuli, bàada ya kuutangazia umma kuwa mkoani kwake hakuna watumishi hewa. Ikulu baada ya kusikia hivyo ikianzisha uchunguzi wake na kugundua kuwa Mkuu huyo wa mkoa "alikurupuka", kwani taarifa yake haikuwa ya kweli. Kufuatia mapungufu hayo, Leo April  11, 2016, Rais Magufuli ametangaza kutengua uteuzi wake kama Mkuu wa mkoa. Halikadhalika Katibu Tawala wa mkoa huo nae amefukuzwa kazi kwa kosa hilohilo, na uchunguzi dhidi yao umeanza.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages