Mbunge
wa jimbo la Vunjo ,James Mbatia akizungumza jambo na Mkurugenzi wa
idara ya Maafa nchini Brigedia Jenerali Mbazi Msuya wakati wakitembelea
kijiji cha Mandaka Mnono kujionea athari ya mafuriko,katikati ni Mbunge
wa viti Maalum (Chadema) mkoa wa Kilimanjaro Lucy Owenya.
Mkurugenzi
wa Idara ya Maafa nchini Brigedia Jenerali ,Mbazi Msuya akimweleza
jambo Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Moshi,Michael Kilawila (wa
tatu kutoka kushoto) wengine ni Mbunge wa jimbo la Vunjo James
Mbatia,Diwani wa kata ya Mabogini Emanuel Mzava .
Baadhi ya wananchi katika kjiji cha Mandaka mnono ambao mashamba yao yameathirika kwa mafuriko.
Sehemu
ya barabara inayounganisha vijiji vya Miwaleni na Mandaka Mnono ikiwa
imeharibika vibaya kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha na
kusababisha mafuriko.
Usafiri wa pikipiki pekee ndio unatumika kuvusha watu kutoka upande mmoja kwenda upande mwingine.
Hivi ndivyo hali inavyoonekana.
Mkurugenzi
wa Idara ya Maafa nchini iliyo chini ya ofisi ya Waziri Mkuu,Mbazi
Msuya akizungumza na wananchi katika eneo hilo lililoharibika vibaya.
Madereva wa bodaboda wakijaribu kupita katika eneo hilo kwa umakini mkubwa.
.
Mbunge wa jimbo la Vunjo ,James Mbatia akitoa maelekezo mara baada ya kutembelea baadhi ya maeneo yaliyoathirika kwa mafuriko.
Kwahisani ya
Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269