Basi hilo lilikuwa likitokea Mbeya mjini kuelekea Tabora kupitia Chunya.
Mkuu wa
Mkoa wa Mbeya, Amos Makala aliyekuwa kwenye shughuli za kusimamia usafi
ameenda kwenda eneo la tukio ili kusaidia uokoaji.
Akizungumza
baada ya kutoka eneo la tukio, amesema waliofariki dunia ni wanaume
wawili na wanawake wawili na mtoto mdogo, ambao bado majina yao
hayajatambuliwa na majeruhi ni 29.
Taarifa
za awali inadaiwa ajali hiyo imesababishwa na gari kufeli breki na kisha
kugonga gema na kupinduka. Dereva aliruka na kutokomea kusikojulikana.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269