Marekani
jana Jumamosi (30.04.2016) imetaka majeshi ya kiongozi wa Syria Bashar
al- Assad kusitisha mashambulizi dhidi ya mji wa Aleppo na kusaidia
kurejesha usitishaji mapigano kwa nchi nzima.
Katika
miito kwa mjumbe maalum wa Umoja wa mataifa nchini Syria na mjumbe wa
upande wa upinzani katika majadiliano, waziri wa mambo ya kigeni wa
Marekani John Kerry amesema umuhimu ni kuhusu usitishaji wa mapigano
utakaodumu nchi nzima.
Usitishaji
mapigano uliitishwa Februari mwaka huu baina ya majeshi ya Assad na
muungano wa waasi lakini umeanza kuporomoka tangu wakati huo, hususan
katika mji uliogawika na uliozingirwa wa Aleppo.
Wiki hii,
Urusi na Marekani zilikubaliana kuzishinikiza pande zinazopigana
kusitisha mashambulizi yao katika majimbo ya Latakia na mashariki ya
Ghouta -- lakini Aleppo iliachwa nje ya makubaliano hayo.
Mashambulizi dhidi ya Aleppo
Mashambulizi
makali ya mabomu yaliendelea katika mji huo, na watu wengi wameuwawa,
na Urusi imeweka wazi kwamba haina nia ya kuyalazimisha majeshi ya
washirika wake kusitisha mapigano.
Wakati
hatua za amani zikionekana kuwa katika wasi wasi mkubwa, Kerry anakwenda
Geneva leo Jumapili (01.04.2016) kwa mazungumzo na mjumbe wa Umoja wa
mataifa Ataffan de Mistura na mawaziri wa mambo ya kigeni wa Saudi
Arabia na Jordan.
Lakini
kwanza, alitumia miito yake kusisitiza kwamba Marekani haijafikiria wazo
la kwamba Aleppo iondolewe katika mpango wa usitishaji mapigano ama
raia wanaweza kushambuliwa.
Katika
miito kwa De Mistura na mratibu mkuu wa kamati ya juu ya upande wa
upinzani kwa ajili ya majadiliano nchini Syria, Riad Hijab, Kerry
ameeleza ,"wasi wasi mkubwa" juu ya Aleppo.
"Waziri
ameweka wazi kwamba kufikisha mwisho ghasia mjini Aleppo na kurejea kwa
hali ya kawaida ya usitishaji mapigano nchi nzima ni suala lililoko
katika umihumu wa juu," msemaji wa wizara ya mambo ya kigeni John Kirby
amesema.(P.T)
Madai ya Urusi
Katika
miito hiyo, Kerry alipuuzia madai ya Urusi na serikali kwamba
mashambulizi mjini Aleppo yanalenga kundi la Al-Nusra Front, kundi la
jihadi ambalo halimo katika mpango wa kusitisha mapigano.
"Utawala
wa Assad unaendelea kuchochea mzozo huu kwa kushambulia raia wasio na
hatia na makundi yanayohusika katika kupunguza uhasama -- na sio Nusra,
kama utawala huo unavyodai," Kirby amesema.
"Mashambulizi
kama hayo yanakwenda kinyume moja kwa moja na usitishaji mapigano na ni
lazima kukomeshwa mara moja," ameeleza. "Waziri wa mambo ya kigeni
amesisitiza kwamba juhudi za awali kuimarisha usitishaji wa uhasama
katika majimbo ya latakia na Ghouta mashariki sio tu kwa maeneo haya
mawili pekee na kwamba juhudi za kurejesha tena usitishaji huo ni lazima
na ni pamoja na Aleppo.
Moja kati
ya mihimili mikubwa ya kiuchumi Aleppo, umeathirika na mapigano mabaya
kabisa katika mzozo huo ambao umewauwa zaidi ya watu 270,000 na wengine
kwa mamilioni wamekimbia makaazi yao.
chanzo:DW
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269