Rais wa
Kenya Jumamosi (30.04.2016) amechoma maelfu ya pembe za ndovu na faru na
kuteketeza mrundiko wa pembe hizo na kutuma ujumbe mkali kwamba
biashara ya viungo vya wanyama haina budi kukomeshwa.
Moshi
ulitanda wakati mrundiko wa pembe hizo ukiteketea katika mbuga ya
wanyama ukingoni mwa mji mkuu wa Nairobi na kuangamiza tani 105 za pembe
kutoka takriban wanyama 8,000 ambao ni uchomaji mkubwa sana wa aina
yake.
Rais
Uhuru Kenyatta amepuuzilia mbali hoja za wale walioitaka Kenya ambayo
ilichoma pembe zake za kwanza hapo mwaka 1989 badala yaake ingeziliuza
pembe hizo ambazo zinakadiriwa kuwa na thamani ya dola milioni 150.
Alisema
kabla ya kutia moto rundo la kwanza la pembe hizo kati karibu ya marundo
kumi na mbili kwamba "Kenya inatowa ujumbe kwamba kwa sisi pembe haina
thamani venginevyo inakuwepo kwa tembo wenyewe."
Kenya yataka marufuku ya pembe(P.T)
Kenya
itataka kupigwa marufuku kabisa kwa mauzo ya pembe duniani wakati wa
Mkutano juu ya Biashara ya Kimataifa kwa Wanyama na Mimea ilioko
hatarini kutoweka iliopangwa kufanyika Afrika Kusini baadae mwaka huu
wakati ujangili ukizidi kuhatarisha wanyama hao.
Mkutano huo wa CITES ulipiga marufuku biashara ya pembe za tembo wa Afrika hapo mwaka 1989 lakini baadae iliruhusu mauzo.
Wito wa Kenyatta wa kupigwa marufuku kwa pembe za tembo umeungwa mkono na Rais Ali Bongo wa Gambia maskani ya tembo wa msituni.
Bongo amesema "kwa majangili wote ,kwa wanunuzi wote, kwa wafanyabiashara wote siku zenu zimemalizika."
Maruku hupunguza mahitaji
Watetezi
wa mazingira wamesema marufuku ya awali ya CITES na uchomaji moto wa
pembe hizo na Kenya hapo mwaka 1989 kumesaidia kupunguza mahitaji na
kutowa faraja kwa tatizo hilo lakini mara baada ya kuruhusiwa mauzo
halali jambo hilo limefufuwa soko lake.
Uwindaji
haramu ilipamba moto kwa miaka mitatu hadi hapo mwaka 2012 wakati
takriban tembo 100,000 waliuwawa sawa na kama tembo 33,000 kwa mwaka.
Katika miaka ya 1970 Afrika ilikuwa na kama tembo milioni moja na laki mbili lakini hivi sasa ina tembo 40,000 hadi 450,000.
Hali ya faru ni mbaya
Hali ya
faru ni mbaya zaidi.Waliobakia Afrika hawazidi 30,00 na jamii moja
inayotambulika kama "Faru Mweupe wa Kaskazini " wako katika hatari ya
kutoweka.Faru hao watatu waliobakia wanahifadhiwa chini ya ulinzi mkali
nchini Kenya.
Kenya
inategemea utalii ambapo wengi huvutiwa katika kambi za kifahari
kutokana na wanyama mashuhuri watano ambao Kenya inajivunia
:tembo,faru,chui,simba na nyati.
Ahadi
zilizolewa na China na Marekani mwaka jana ambazzo ni masoko makuu
mawili ya pembe za kuweka marufuku ya moja kwa moja ya kuagizia na
kusafirisha pembe zimesaidia kuangusha bei za pembe.
Lakini
bei za pembe za faru bado zinaendela kupanda. Doria za askari wa wanyama
pori wenye silaha katika hifadhi na hatua nyengine zimesaidia kudhibiti
uwindaji haramu kwa kiasi fulani lakini mustakbali wa mnyama huyo bado
uko hatarini.
Katika
miaka ya 1970 Kenya ilikuwa na faru 20,000 na kupunguwa hadi kufikia 400
katika miaka ya 1990.Hivi sasa ina takriban faru weusi 650 na
inawahifadhi faru weupe watatu wa kaskazini wakati wanasayansi
wakishindana na wakati kutafuta mbiu ya kuwapandikiza uzazi.
Chanzo:DW
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269