Jumba lililoanguka
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta ametaka kukamatwa kwa mmiliki wa nyumba ilioanguka mjini Nairobi na kuwaua watu saba.
Kenyatta
aliyezuru mkasa wa tukio hilo pia amewataka wakaazi wa nyumba zilizopo
karibu na eneo hilo kuondoka wa kuwa nyumba hizo zimethibitishwa
kutokuwa salama.
Maafisa
wa Kaunti ya Nairobi wamethbitisha kuwa nyumba hiyo ilikuwa
imeorodheshwa miongoni mwa majumba yaliotarajiwa kuvunjwa kwa kuwa
haikuafikia viwango vya nyumba ya kuishi watu wengi.
Rais Uhuru Kenyatta
Juhudi za uokoaji zinaendelea lakini zimetatizwa na mvua kubwa inayoendelea mbali na uwezo wa kufikia eneo hilo.
Jeshi la
Kenya linaloongoza juhudi hizo za uokozi limelazimika kutumia mikono na
misumeno ya kielektroniki kuchimba chini ya vifusi kwa kuwa vifaa
vinavyohitajika katika zoezi hilo haviwezi kuingia katika eneo hilo.BBC
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269