Breaking News

Your Ad Spot

May 22, 2016

MALI WAANDAMANA KUPINGA UFISADI WA KUCHUPA MIPAKA WA VIONGOZI WA SERIKALI

Maelfu ya raia wa Mali wamefanya maandamano makubwa mjini Bamako, mji mkuu wa nchi hiyo kulalamikia utendaji duni wa serikali na ufisadi mkubwa wa viongozi wa serikali.
Waandamanaji waliokuwa wamebebelea bendera zilizokuwa zimeandikwa nara za kulaani ongezeko la kiwango cha juu cha ufisadi nchini humo, wametaka kufanyika mabadiliko katika muundo wa kiuchumi na kadhalika kuondoka madarakani Rais Ibrahim Boubacar Keïta wa nchi hiyo ambaye amekuwa madarakani tangu mwaka 2013. Baadhi ya waandamanaji walipiga nara zenye kauli kali dhidi ya serikali kutokana na miamala mibaya inayofanywa na maafisa wa usalama na polisi ya nchi hiyo. Kadhalika waandamanaji wametoa ripoti ya kutaka kukomeshwa ongezeko la ufisadi wa kifedha na kiuchumi nchini humo, na kadhalika hatua zisizofaa za serikali. Itakumbukwa kuwa, nchi ya Mali iliyo magharibi mwa Afrika, ni moja ya nchi masikini zaidi duniani. Mbali na matatizo ya kiuchumi, Mali inakabiliwa pia na ukosefu wa usalama unaosababishwa na makundi ya wanamgambo wanaotaka kujitenga na nchi hiyo.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages