Breaking News

Your Ad Spot

May 22, 2016

WAZIRI ALIYEPIGWA KALAMU NYEKUNDU NA RAIS MAGUFULI KWA ULEVI, AENDELEA KUSAKAMWA NA TUHUMA

Ikiwa ni siku moja baada ya Waziri wa Mambo ya Ndani nchini Tanzania, Charles Kitwanga kupigwa kalamu nyekundu na Rais John Pombe Magufuli kutokana na ulevi, wanasiasa na wasomi mbalimbali nchini humo wameendelea kumbana zaidi wakisema hatua hiyo ya rais imekuja ikiwa imechelewa.
Hayo ni baada ya wapinzani kumtaka Rais Magufuli kumuondoa mapema kwenye nafasi hiyo kutokana na Kitwanga kuhusishwa na Kampuni ya Infosys ambayo ilitoa ushauri kwa Kampuni ya Lugumi Enterprises iliyopewa zabuni ya kufunga vifaa vya kuchukua alama za vidole (AFIS) katika vituo vya polisi. Kwa upande wake, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema uamuzi huo wa kutimuliwa Kitwanga ulikuwa sahihi na kwamba, swali ambalo Kitwanga hakulijibu vizuri kutokana na hali ya ulevi, litapaswa kujibiwa upya baada ya wabunge kuomba mwongozo wa swali hilo. Waziri mkuu huyo ameongeza kuwa, Rais Magufuli ametengua uteuzi wa waziri huyo Kitwanga kuanzia juzi. Wabunge wa chama tawala CCM na wale wa upinzani wameitaja hatua hiyo ya rais wa Tanzania kuwa ilikuwa haki kwa waziri kuachishwa kazi kwani alitia aibu serikali.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages