Mtaalamu
kutoka Marekani, Dk Brian McMahon akizungumza na madaktari na wauguzi
wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) kuhusu tiba ya homa sugu ya ini
inayosababishwa na virusi vya Hepatitis B.
Dk
Aaron Haris kutoka Marekani akielezea jinsi mradi huo
utakavyowanufaisha Watanzania ambao wameambukizwa virusi vya vya
Hepatitis B.
Dk
Edwin Masue wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) akiwasilisha mada
kuhusu dalili za homa sugu ya ini inayosababishwa na virusi vya
Hepatitis B.
Madaktari na wauguzi wakimsikiliza Dk McMahon wakati akielezea kuanza kwa mradi wa tiba ya homa ya ini kwa watu mbalimbali.
Mkuu wa Idara ya Magonjwa ya Tumbo, Dk John Rwegasha (kushoto)
akifuatilia mada iliyowasilishwa na Dk Edwin Masue na Dk Eva Uiso wa
Hospitali ya Taifa ya Muhimbili. Wengine ni Dk McMahon na Dk Haris
kutoka Marekani.
………………………………………………………………………….
Na Neema Mwangomo-MNH.
Hospitali
ya Taifa Muhimbili-MNH-inatarajia kuanza kampeni ya kupima na kutoa
tiba kwa ugonjwa wa Homa Sugu ya Ini ambao unasababishwa na Virusi
vya HEPATITIS B .
Daktari
Bingwa wa magonjwa ya Mfumo wa Chakula na Ini katika Hospitali ya
Taifa Muhimbili, Edwin Masue amesema kundi la ndio limeonekana
kuathirika zaidi kwa kuwa mtoto anapata maambukizi kutoka kwa mzazi .
Kwa
mujibu wa Dk. Masue mtoto anapozaliwa lazima apatae chanjo, na pia
mama mjamzito ambaye anagundulika kuwa ana Virusi vya HEPATITIS B
hupatiwa dawa ya kumkinga mtoto katika miezi mitatu ya mwisho kabla ya
kujifungua .
“Tuangalie
uwezekano ili watu waelewe tatizo hili mapema , wapime na wawahi kupata
matibabu kwani maambukizi makubwa yanatoka kwa mama kwenda mtoto na
kwa wale wanaoanza kutumia dawa za VVU wanatakiwa kupima ugonjwa wa homa
ya Ini kwa kuwa virusi vinaingiliana,” amesema Dk . Masue .
Mkakati wa MHN.
Kwa
upande wake Daktari John Rwegasha amesema katika kipindi cha Julai
mwaka huu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili kutaanzishwa mradi wa
miaka mitano ambao unalenga kupima na kutibu watu ambao watagundulika
kuwa na homa sugu ya ini na kwamba hata baada ya kukamilika kwa mradi
huo wananchi wataendelea kupatiwa matibabu bure .
“
Kuna muongozo wa tiba wa Shirika la Afya Duniani-WHO- ambao umetolewa
mwaka jana hivyo tunataka kuangalia matumizi ya huo muongozo kwenye nchi
zetu za Dunia ya tatu , kuna watu wametusaidia tulikuwa hatuna uwezo wa
dawa. Awali tulikuwa tunaazima dawa kwenye mradi wa HIV hivyo kupitia
mradi huo tutakuwa na dawa pamoja na vitenganishi vya kimaabara,”
amesema Dk Rwegasha.
“Kati
ya watu 100, wanane wanatembea na ugonjwa huo bila kufahamu baada ya
miaka 20 mtu anapata matatizo ya ini na kusababisha ini kushindwa
kufanya kazi na tumbo kuvimba hivyo natumia fursa hii kuwaambia
wananchi wajitokeze kupima mapema ili waweze kupatiwa matibabu,”
amesema.
Virusi vinavyoenea:
Kwa
mujibu wa watalaam , asilimia kubwa ya Virusi vya HEPATITIS B vipo
kwenye damu , mbegu za kiume , ute wa mwanamke na hedhi ya mwanamke na
kwamba maambukizi yake hayana tofauti na maambukizi ya Virusi vya
Ukimwi .
Dalili za ugonjwa huo:
-Kichefuchefu
-Kukosa hamu ya kula
-Macho kua ya njano
-Mkojo kuwa wa njano
-Kupata choo chenye rangi ya njano ambayo imepauka
-Mwili mzima kuishiwa nguvu.
Hata hivyo dalili hizo si zote zinaenda pamoja , kuna wengine huwa hawana dalili hizo kabisa .
tuna ombamusada mikowani tulisha pima tukakutwa natatizo hili Mbeya
ReplyDelete