Mtendaji
Mkuu wa Temesa Mhandisi Manase Ole-Kujan akitoa taarifa juu ya
kusimamia kwa huduma za Mv Magogoni inayofanyiwa Matengenzo makubwa.
Wananchi
wakipita katika daraja la Nyerere lilopo Kigamboani Jijini Dar es
Salaam mara baada ya kuzinduliwa rasmi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe. Dkt John Pombe Magufuli hivi karibuni.
Kivuko cha Mv Magogoni kikiwa katika shughuli zake za kila siku za kutoa huduma kwa wananchi. (Picha na Raymond Mushumbusi MAELEZO)
Na mwandishi Maalum
Na mwandishi Maalum
Kivuko
cha Mv Magogoni kinachotoa huduma kwa wananchi kutoka upande wa bahari
eneo la Magogoni kuelekea Kigamboni Jiji la Dar es Salaam kimesitisha
kutoa huduma kwa ajili ya kufanyiwa matengenezo makubwa.
Katika
taarifa iliyotolewa na Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na
Umeme(TEMESA) Mhandisi Manase Ole Kujan kwa niaba ya Wizara ya
Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano imesema kuwa kuanzia Mei 5 2016 kivuko
hicho kitakuwa katika matengenezo makubwa ambayo yatafanya kusitisha
huduma zake kwa muda.
Taarifa
hiyo imesema kuwa huduma za kivuko zitaendelea kama kawaida kwani
wananchi watatumia huduma ya kivuko cha Mv Kigamboni pamoja na kivuko
kilichokodishwa na Serikali kutoka kampuni ya Azam Marine vitavyokuwa
vinasaidia kutoa huduma kwa wananchi kwa muda wote ambao Mv Magogoni
itakuwa katika matengenezo.
“ Muda
wake wa matengenezo umefika na ni wakati muafaka kwa kivuko kwenda
kwenye matengenezo ni muda mrefu kimetumika na kusimama kwa kivuko hiki
hakutaleta madhara makubwa kwani mara baada ya kuzinduliwa kwa daraja la
Nyerere hivi karibuni tuna imani wananchi watatumia daraja hili ili
kendelea na shughuli zao za kila siku” imesema taarifa hiyo.
Kwa
mujibu wa taarifa hiyo wananchi wenye magari wanaotumia vivuko hivyo
wameshauriwa kutumia daraja jipya la Nyerere ili kuepukana na usumbufu
wa kusubiri kivuko pekee cha Mv Kigamboni chenye uwezo wa kubeba magari
na kufafanua kuwa kivuko kutoka Azam Marine kina uwezo wa kubeba watu
peke yake.
Taarifa
hiyo imeendelea kusema kuwa matengenezo ya kivuko cha Mv Magogoni
yatafanyika Jijini Dar es Salaam chini ya usimamizi wa Temesa katika
matengenezo ya mitambo na ukarabati na ujenzi utafanywa na kampuni ya
kizawa ya na Songoro Marine Transport Yard yenye makao makuu yake Jijini
Mwanza.
Aidha
kivuko cha Mv Magogoni kitakabidhiwa kesho kwa kampuni ya Songoro Marine
Transport Yard kwa ajili ya matengenzo hayo na mara baada ya mkandarasi
kuangalia hali ya kivuko atatoa muda kamili wa kumalizika kwa
matengenezo ya kivuko hicho.
Serikali
katika katika jitihada za kupunguza msongamano katika vivuko hivyo
imeamua kwenda kukifanyia ukarabati mkubwa ili kukiongezea uwezo na
ufanisi wa kuhudumia wananchi kwa kusaidiana na daraja jipya la Nyerere
lililozinduliwa na Mhe. Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt john
Pombe Magufuli hivi karibuni ili kuondoka na tatizo la msongamono
kwenye vivuko vya Kigamboni.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269