Spika
wa Bunge Mhe. Job Ndugai akilihutubia Bunge la Afrika (Pan African
Parliament) kuwasilisha Ujumbe wa Mshikamano kwa wabunge wa Bunge hilo
wakati wa Ufunguzi wa rasmi wa Mkutano wa Pili wa Bunge hilo uliofanyika
Mjini Midrand Afrika Kusini. Mhe. Ndugai alikuwa miongoni mwa viongozi
mashuhuri 12 kutoka Barani Afrika walioalikwa kutoa ujumbe huo kwa
wabunge wa Afrika.
Spika
wa Bunge Mhe. Job Ndugai akilihutubia Bunge la Afrika (Pan African
Parliament) kuwasilisha Ujumbe wa Mshikamano kwa wabunge wa Bunge hilo
wakati wa Ufunguzi wa rasmi wa Mkutano wa Pili wa Bunge hilo uliofanyika
Mjini Midrand Afrika Kusini. Mhe. Ndugai alikuwa miongoni mwa viongozi
mashuhuri 12 kutoka Barani Afrika walioalikwa kutoa ujumbe huo kwa
wabunge wa Afrika.
Spika
wa Mhe. Job Ndugai akiwa na baadhi ya Maspika wenzie kutoka mabunge ya
Nchi za Bara la Afrika kwenye Mkutano wa Bunge la Afrika (Pan African
Parliament) alikoalikwa kuwasilisha Ujumbe wa Mshikamano kwa wabunge wa
Bunge hilo wakati wa Ufunguzi wa rasmi wa Mkutano wa Pili wa Bunge hilo
uliofanyika Mjini Midrand Afrika Kusini. Mhe. Ndugai alikuwa miongoni
mwa viongozi mashuhuri 12 kutoka Barani Afrika walioalikwa kutoa ujumbe
huo kwa wabunge wa Afrika. Kulia kwake ni Spika wa Bunge la Seneta la
Lesotho Mhe Seeiso Berenge Seeiso na kushoto ni senate kutoka Bunge la
Afrika Mhe. Bennette hayatoe
Wabunge
wa Bunge la Afrika wanaowakilisha Tanzania wakila kiapa cha uaminifu.
Kutoka kushoto ni Mhe. Asha Abdalah Juma, Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile,
Mhe. David Silinde na Mhe. Mboni Mhita.
Na Owen Mwandumbya, Midrand Afrika Kusini.
Spika
wa Bunge la Tanzania Mhe. Job Ndugai amesema ili Bara la afrika liweze
kuwa Bara lenye nguvu kiuchumi na sauti ya maamuzi duniani halina budi
kujikita katika umoja na mshikamono.
Mhe. Ndugai aliyasema hayo alipokuwa akilihutubia Bunge la Afrika
(Pan African Parliament) leo kuwasilisha Ujumbe wa Mshikamano kwa
wabunge wa Bunge hilo wakati wa Ufunguzi wa rasmi wa Mkutano wa Pili wa
Bunge hilo uliofanyika Mjini Midrand Afrika Kusini.
Akizungumzia changamoto zinazolikabli bara la Afrika Mhe. Nduagi
alisema nchi nyingi barani Afrika zinakabiliwa na matatizo yanayolingana
ambayo ni Vita vya wenyewe kwa wenyewe, ugaidi, umasikini na mengineyo
ambayo yanahitaji suluhisho la Pamoja kuyakabili..
“ katika duniani ya sasa ni vyema tukakabiliana na changamoto
zinazotukabili kwa pamoja. Matajiri hawawezi kuepuka athari za umasikini
na ukosefu wa amani. Kinachotokea eneo moja kinaathiri maeneno mengi
mathalani vita vya wenyewe kwa wenyewe Somalia imesababisha wakimbizi
katika maeneo mengi duniani” alisema Ndugai
Akizungumzia nafasi ya wabunge katika kupiga vita changamoto
zinazolikabili bara la Afrika, Mhe. Ndugai amesema wabunge wa Bunge la
Afrika kama wawakilishi wa Manbunge ya Nchi wanachama wa Umoja wa Afrika
wanawajibu wa kutetea maslahi ya Bara la Afrika bila kujali itikadi za
kisiasa, maeneo wanayotoka na mambo mengine yanayoweza kuligawa bara la
Afrika.
“ Mkiwa Wabunge mnaowakilisha nchi zenu katika Bunge hili, nilazima
mhakikishe Umoja wa Afrika unasimamia ipasavyo masalahi ya bara la
Afrika ili kutimiza ndoto waliokuwa nayo waasisi wa umoja huu wa Afrika.
Kwa mfano baba wa Taifa la Tanzania Mwalimu Julius kambarage Nyerere
alisema lazima tukimbie wakati wengine wakitembea” aliongeza Ndugai
Mapema akitoa salamu za Bunge la Lesotho, Spika wa Bunge la Nchi hiyo
Mhe. Nthloi Motsamai alisifu juhudi za Mwalimu Julius Nyerere pamoja na
waasisi wengine wa bara hili katika kuimarisha umoja wa Afrika na
kuwataka wabunge wa Bunge la afrika kuhakikisha mawazo ya viongozi hawa
ya kulifanya bara la afrika kuwa moja yanatimia.
Katika hatua nyingine, wabunge wa Tanzania wanaowakilisha Tanzania
katika Bunge la Afrika walikula kiapo cha uaminifu kuwa wabunge wa Bunge
hilo baada ya Bunge la Tanzania kuwachagua mapema mwezi Januari.
Wabunge hao ni pamoja na Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile, Mhe. Mboni
Mhita, Mhe. David Silinde na Mhe. Asha Abdalah Juma. Mhe. Ndugai
anatarajia kurejea nchini kesho jumatano ambapo Bunge la Afrika
linaendelea na Vikao vyake hadi tarehe 13 Mei, 2016.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269