Breaking News

Your Ad Spot

May 31, 2016

NAIBU SPIKA DKT. TULIA ACKSON AKUTANA NA WAANGALIZI WA UCHAGUZI KUTOKA JUMUIYA YA ULAYA

Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Dkt. Tulia Ackson (kulia) akizungumza jambo na Waangalizi wa Uchaguzi uliofanyika Oktoba 25, mwaka jana (2015), kutoka Umoja wa Ulaya. Judith Sargentini (kushoto) na Balozi wa Umoja huo  . Roeland Van De Geer (katikati) waliofika Ofisini kwake Dodoma leo Mei 31, 2016.
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Tulia Ackson akiwasikiliza waangalizi wa Uchaguzi Mkuu kutoka Umoja wa Nchi za Ulaya (EU) waliofika Ofisini kwake kuwasilisha Taarifa ya Umoja huo kuhusu Uchaguzi Mkuu uliofanyika nchini Oktoba 25, 2015.
Waangalizi wa Uchaguzi Mkuu kutoka Umoja wa Nchi za Ulaya (EU) wakizungumza na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Tulia Ackson (hayupo pichani) ofisini kwake Dodoma.
Balozi wa Umoja wa Ulaya Mhe. Roeland Van De Geer (kulia) akimkabidhi Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. Tulia Ackson Taarifa  ya miradi inayotekelezwa na Umoja wa Ulaya nchini Tanzania.


Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.Tulia Ackson (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Waangalizi wa Uchaguzi  kutoka Umoja wa Nchi za Ulaya (EU) waliomtembelea Ofisini kwake leo mjini Dodoma. (PICHA NA ARON MSIGWA NA FATMA SALUM-MAELEZO).

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages