Breaking News

Your Ad Spot

May 31, 2016

RAIS KENYATTA AKUTANA NA RAILA ODINGA

Raila Odinga
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta anafanya mazungumzo na kiongozi wa upinzani nchini humo Raila Odinga ili kuondoa wasiwasi wakati ambapo taifa hlo linajiandaa kwa uchaguzi mwaka mkuu ujao.
Bw Odinga alikatiza ziara yake ya kushiriki katika mazishi kusini magharibi mwa eneo la Natol ili kuhudhuria mkutano huo wa Uhuru Kenyatta katika mji mkuu wa Nairobi.
''Nilipokea simu kutoka ikulu ya mkutano na rais Uhuru Kenyatta.Naomba ruhusa yenu watu wa Narok nielekee kuzungumza naye,alinukuliwa na gazeti la Daily Nation akiwaambia waombolezaji.Nitatangaza kwa Wakenya iwapo tumekubaliana na iwapo hatujakubaliana pia nitawaelezea'', aliongezea bw Odinga.
Uhuru Kenyatta
Muungano wa upinzani nchini Kenya Cord umeapa kuhudhuria mkutano jijni Nairobi hapo kesho,licha ya kwamba serikali ilitangaza kupigwa marufuku.
Watu kadhaa wameuawa katika ghasia kati ya polisi na wafuasi wa upinzani wanaopigania mabadiliko ya sheria ya kupiga kura. BBC

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages