Breaking News

Your Ad Spot

May 5, 2016

REAL MADRID WAICHAPA MAN CITY BAO 1-0 NA KUTINGA FAINALI YA LIGI YA MABINGWA ULAYA


Real Madrid imefanikiwa kufuzu kucheza fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya itakayochezwa Mei 28 jijini Milan, Italia.
Madrid imetinga fainali baada ya kuitwanga Man City kwa bao 1-0 katika mechi ya pili ya nusu fainali iliyopigwa kwenye Uwanja wa Santiago Bernabeu jijini Madrid.
Bao la Madrid limepatikana baada ya shuti la Gareth Bale aliyekuwa akipiga krosi kumgonga Fernando na kujaa wavuni.

Pamoja na Madrid kutinga fainali, maana yake Kocha Zinedine Zidane ameandika rekodi yake ya kwanza kucheza fainali hiyo, safari hii akiwa kocha. Lakini Man City imeishia nusu fainali iliyokuwa ni mara ya kwanza kwake kuingia
Ushindi huo wa bao 1-0, unaipitisha Madrid hadi fainali baada ya sare ya bila bao katika mechi ya kwanza jijini Manchester.











No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages