Wafanyakazi watatu wa Shirika la Msalaba Mwekundu wakombolewa DRC
Shirika la Msalaba Mwekundu limesema kuwa,
wafanyakazi watatu wa shirika hilo waliokuwa wametekwa nyara mashariki
mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wamekombolewa.
Shirika la habari la Ufaransa AFP limemnukuu Alessandra
Menegon, mkuu wa kazi za Shirika la Msalaba Mwekundu nchini DRC akisema
leo mjini Kinshasa kuwa amefurahishwa sana na kuona wafanyakazi hao
wamerejea kwa familia zao. Vile vile amewashukuru viongozi wa serikali,
wananchi na wakuu wa kikabila na kidini kwa msaada wao uliofanikisha
kukombolewa wafanyakazi hao.
Kwa upande wake, Elisabeth Cloutier, msemaji wa Shirika la Msalaba
Mwekundu mjini Goma, makao makuu ya mkoa wa Kivu Kaskazini huko
mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo amesema kuwa, hakuna
fedha zozote zilizotolewa kwa ajili ya kukombolewa wafanyakazi hao.
Wiki iliyopita, Shirika la Msalaba Mwekundu lilitangaza habari ya
kutekwa nyara wafanyakazi wake watatu na watu wenye silaha wasiojulikana
katika eneo la Rutshuru katika mkoa wa Kivu Kaskazini.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269