Rais Bashar al Assad wa Syria ameishukuru serikai na taifa la Iran kwa uungaji mkono wake kwa wananchi na serikali ya nchi yake.
Rais Assad amesema hayo leo mjini Damascus wakati alipoonana na
Ali Akbar Velayati, Mshauri wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya
Kiislamu na kuongeza kuwa: Ninamshukuru sana Kiongozi Muadhamu wa
Mapinduzi ya Kiislamu, wananchi na serikai ya Iran kwa uungaji mkono wao
kwa wananchi na serikali ya Syria.
Aidha amegusia vita vya miaka minane ilivyolazimishwa kupigana Iran
baada ya kuvamiwa na utawala wa wakati huo wa Iraq na kusema kuwa: Sisi
hatuwezi kusahau uvumilivu na kusimama kidete wananchi wa Iran katika
vita hivyo vya kulazimishwa.
Amesema: Kiongozi Muadhamu, wananchi na serikali ya Iran, inatumia
suhula zake zote katika kukabiliana na magaidi na makundi yenye misimamo
mikali inayokufurisha Waislamu wengine na tuna matumaini makubwa ya
kuyashinda makundi hayo ya kitakfiri. Amesema: Ninatumia fursa hii
kutuma shakrani zangu za dhati kwa Kiongozi Muadhamu, kwa serikali na
kwa wananchi wa Iran kwa kuwa pamoja na taifa la Syria.
Kwa upande wake Dk Velayari amemwambia Rais Bashar al Assad kwamba:
Kujihami kishujaa wananchi na serikali ya Syria kwa uongozi wako wewe ni
kitu ambacho hakijawahi kutokea katika historia na ijapokuwa vita vya
Syria vina panda shuka nyingi lakini kwa uongozi wako na kwa taufiki ya
Mwenyezi Mungu, hatimaye taifa na serikali ya Syria itashinda tu, na
kwamba Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu anakuombeeni dua
wakati wote ili mpate ushindi wa haraka katika vita hivi.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269