
Shambulizi katika Hoteli ya Naasa Hablood mjini Mogadishu Somalia 25 06 2016
Takriban
watu 11 wameuawa jana Jumamosi katika shambulizi kwenye hoteli ya mjini
Mogadishu nchini Somalia ambalo linadaiwa kutekelezwa na wanamgambo wa
Al Shabaab.
Shambulizi
hilo ambalo ni la karibuni katika mfululizo wa mashambulizi
yanayotekelezwa na kundi la Al Shabab kulenga hoteli na migahawa,
lilianza wakati mshambuliaji wa kujitoa mhanga alipolipua bomu
lililokuwa limetegwa garini nje ya jengo la hoteli.
Watu
wenye silaha walivamia hoteli iitwayo Naasa Hablood na milio ya risasi
ilisikika kwa saa kadhaa, mashahidi wamesema, kabla ya mamlaka kutangaza
mashambulizi kumalizika.
Vikosi maalum vya usalama vimekomesha shambulizi hilo baada ya kuwaua washambuliaji watatu ndani ya hoteli.
Msemaji
wa wizara ya usalama Abdi Kamil Shukri, amewaambia waandishi wa habari
kuwa raia kumi na mmoja, wawili kati yao madaktari, wameuawa katika
shambulio hilo.RFI
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269