Breaking News

Your Ad Spot

Jun 26, 2016

MTEMVU ADAI KUIBIWA NYARAKA ZA UCHAGUZI OFISINI KWAKE

Abbas Mtemvu
 Aliyekuwa Mbunge jimbo la Temeke, Jijini Dar es Salaam, kwa tiketi ya CCM,  Abbas Mtemvu, amedai kuibiwa mali mbalimbali na nyaraka za uchaguzi mkuu uliopita.

Akizungumza jijini Dar es Salaam, Mtemvu amedai kuwa wizi huo umefanywa kwa nyakati tofauti na watu wasiojulikana na kwamba wizi huo umekuwa aukifanyika katika ofisi yake iliyopo mtaa wa Jamhuri katikati ya Jiji la Dar es Salaam.

 Alisema Machi 18, 2016, watu wasiojulikana walifika kwenye ofisi yake iliyopo Chang'ombe na baada ya kumpa mlinzi dawa za kulevya walivunja mlango na kuiba mali mbalimbali televisheni tatu, laptop mbili, ipad mbili, kamera mbili za digital, feni kubwa mbili, simu aina ya Huwawei 330 na begi lenye nyaraka za uchaguzi.

Jana pia wezi walifika katika ofisi yake iliyopo Chang'ombe na kuiba Pikipiki tatu, viroba vitatu vya mchele makasha matano ya tambi.

Mlinzi aliyedai kulishwa dawa za kulevya ameshikiliwa na polisi katika kituo cha Temeke kwa ajili ya kumhoji zaidi  
   Abbas Kilapo (aliye vaa kofia) akiwaonyesha Askari kanzu wa Kituo cha Chang'ombe jinsi watuhao walivyofanikiwa kuondoka na vitu hivyo
 Muhusika wa ofisi hiyo Abbas Kilapo akiwaonyesha Askari Kanzu na waandishi wa hapari Namba za pikipiki na kadi za Pikipiki zilizo ibwa na watu wanaodaiwa ni wezi
  Abbas Kilapo akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kufika Ofisini hapo
 Katibu mwenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Kata ya Miburani, Ally Kamtande akimpepea mlinzi huyo leo. (PICHA ZOTE NA KHAMISI MUSSA 

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages