
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.
John Pombe Magufuli akisalimiana na Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Aboubakar
Zubeir Ikulu jijini Dar es Salaam. Rais Dkt. Magufuli amefuturisha makundi
mbalimbali ikiwemo viongozi wa dini, chama Serikali ya mkoa, Watoto Yatima na
wenye ulemavu wa ngozi Albino, Wavuvi wa ferry, walemavu vya viungo pamoja na
wafanyakazi wa Ikulu.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.
John Pombe Magufuli akizungumza na Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Aboubakar
Zubeir wakati wakielekea kufuturu Ikulu jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkuu
wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda na Sheikh Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam
Alhadi Mussa Salum.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.
John Pombe Magufuli akizungumza na Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Aboubakar
Zubeir mara baada ya kufuturu na makundi ya watu mbalimbali Ikulu jijini Dar es
Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.
John Pombe Magufuli akizungumza na makundi mbalimbali (hawapo pichani)ikiwemo
viongozi wa dini, chama Serikali ya mkoa, Watoto Yatima na wenye ulemavu wa
ngozi (Albino),walemavu wa viungo pamoja na wafanyakazi wa Ikulu mara baada ya
kuwafuturisha Ikulu jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa kwenye foleni ya kupata
futari pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda Ikulu jijini Dar es
Salaam.

Baadhi ya wananchi wakifatilia kwa makini hotuba
ya Rais wa Jamhuri ya Muungano Dkt. John Magufuli Ikulu jijini Dar es Salaam

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.
John Pombe Magufuli akiwa na Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Aboubakar Zubeir , Sheikh Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Alhadi
Mussa Salum pamoja Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda wakiwa wamesimama
wakati wa dua mara baada ya kufuturu

Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimsikiliza mtoto mwenye
ulemavu wa ngozi aliyetambulika kwa jina moja la Yusuph mara baada ya
kuwafuturisha Ikulu jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.
John Pombe Magufuli akiagana na baadhi ya makundi ya akina mama waliojumuika
katika futari hiyo.

Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na baadhi ya
watoto wenye ulemavu wa ngozi (Albino) mara baada ya kuwafuturisha Ikulu jijini
Dar es Salaam

Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Rev Vernon Fernandes
wa kanisa la Agape mara baada ya
kufuturu pamoja na makundi mbalimbali ya wananchi Ikulu jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa pamoja na Mufti Mkuu wa
Tanzania Sheikh Aboubakar Zubeir mara
baada ya kumaliza tukio la kufuturisha makundi hayo Ikulu jijini Dar es Salam. PICHA NA IKULU
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269