
Rais
wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph akikagua kituo cha
mawasiliano ya polisi (Call centre) katika kituo cha Kati jijini, Dar es
salaam
wakati wa uzinduzi wa Kitaifa wa Kituo cha Mawasiliano cha Jeshi la
Polisi, wa nne kushoto ni Waziri wa mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba,
wasaba kushoto ni Katibu Mkuu
Wizara ya mambo ya Ndani Meja Jenerali Projest Rwegasira, wakwanza
kushoto ni IGP Ernest
mangu, Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam na watatu ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es
Salaam, Paul Makonda na viongozi wengine wa
sekta ya umma na binfasi.(PICHA NA IKULU)

Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph akizindua Kituo kidogo
cha Polisi kinachohamishika wakati wa uuzinduzi wa Kitaifa wa Kituo cha
Mawasiliano cha Jeshi la Polisi (Call Centre) katika viwanja vya Biafra
jijini Dar es salaam. wapili kushoto ni Rais Mstaafu Dkt Jakaya Mrisho Kikwete,
Waziri wa mambo ya Ndani Mwigulu Nchemba (kulia), Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda

JONAS KAMALEKI, MAELEZO
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John
Pombe Magufuli amelitaka jeshi la polisi nchini kuwadhibiti majambazi ipasavyo
kwa kuwanyanganya silaha kwenye matukio ya kiuharifu ili kukomesha vitendo
viovu katika Taifa.
Rais Magufuli ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati wa
uzinduzi wa Mpango wa Usalama wa Jamii.
“Inashangaza jambazi anavamia kituo cha polisi anaua na
anaondoka wakati polisi wapo na wana silaha na risasi wanazo lakini wanashindwa
kumnyang’anya silaha,”alishangaa Rais Magufuli.
Ameongeza kuwa ujambazi na vitendo vya uharifu nchini inabidi
vikomeshwe mara moja ili watanzania waishi kwa amani na kufanya maendeleo kwani
wananchi wanataka maendeleo.
Akiongelea kuhusu maslahi na vitendea kazi kwa jeshi la polisi,
Rais Magufuli amesema kuwa serikali yake itafanya kila iwezalo kuliwezesha
jeshi hilo ili liweze kufanya kazi kwa ubora zaidi.
Rais Magufuli ameonyesha kuwa na imani na jeshi la polisi licha
ya kuwa na kasoro ndogo ndogo kwa baadhi ya polisi ambao wanalichafua jeshi
hilo.
Aidha ametoa agizo kwa TCRA kushirikiana na jeshi la polisi
nchini ili kuweza kurekodi simu na kutoa print out mara moja
tofauti na ilivyo sasa.
Kuhusu kundi la wafanyakazi wanaofanyakazi kwenye Dawati la
Taarifa la polisi, Mhe. Rais amemtaka Mkuu wa Jeshi hilo, IGP Ernest Mangu
kuwafikiria na kuwapatia posho ya kazi kwani kazi wanayoifanya ni ngumu mno na
inahitaji umakini zaidi.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda
amemwomba Mhe. Rais kuliongezea fedha jeshi hilo ili liweze kufanya kazi kwa
ustadi zaidi na kukomesha vitendo vya uharifu nchini.
Makonda amelipongeza jeshi la polisi kwa kudhibiti matukio ya
ujambazi hapa nchini hususani kwenye mabenki.
Mpango huu wa Usalama wa Jamii umezinduliwa leo na utadumu hadi
2019 na unatarajiwa kutoa matokeo makubwa ya kudhibiti uharifu nchini.

Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph akimkabidhi tuzo ya
ufadhili Bi. Edna Rajabu wa kwa niaba ya Shirika la Utangazaji la
TBC wakati wa uzinduzi wa Kitaifa wa Kituo cha Mawasiliano cha Jeshi
la Polisi katika viwanja vya Biafra jijini Dar es salaam leo. Waziri wa mambo ya Ndani Mhe Mwigulu
Nchemba (wakwanza kushoto), Katibu Mkuu kiongozi Mhe. John Kijazi (watatu kulia), IGP Ernest manu, Mkuu wa
Mkoa wa Dar es salaam Mhe Paul Makonda na viongozi wengine wa sekta ya
umma na binfasi.

Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph akimkabidhi tuzo ya
ufadhili Mkurugenzi Mtendaji wa TBA . Elius Mwakalinga wakati
wa uzinduzi wa Kitaifa wa Kituo cha Mawasiliano cha Jeshi la Polisi
katika viwanja vya Biafra jijini Dar es salaam leo. Waziri wa mambo ya Ndani Mhe Mwigulu
Nchemba, Katibu Mkuu kiongozi Mhe. John Kijazi, IGP Ernest mangu, Mkuu wa
Mkoa wa Dar es salaam Mhe Paul Makonda na viongozi wengine wa sekta ya umma
na binfasi.


Kiongozi wa chama cha UPDP, Fahmi Dovutwa, akisalimia wananchi

Rais
wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph akisimama wakati
wa wimbo
wa Taifa wakati wa uzinduzi wa Kitaifa wa Kituo cha Mawasiliano cha
Jeshi
la Polisi katika viwanja vya Biafra jijini Dar es salaam leo. akiwemo
Rais Mstaafu Dkt Jakaya Mrisho Kikwete(wa tatu kushoto), Waziri wa mambo
ya Ndani Mhe Mwigulu
Nchemba, Katibu Mkuu kiongozi Mhe. John Kijazi, IGP Ernest mangu, Mkuu
wa
Mkoa wa Dar es salaam Mhe Paul Makonda na viongozi wengine wa sekta ya
umma na binfasi.

Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph akihutubia uzinduzi
wa Kitaifa wa Kituo cha Mawasiliano cha Jeshi la Polisi katika viwanja
vya Biafra jijini Dar es salaam leo. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendajiw a
Superdoll, Seif Ali Seif.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269