Breaking News

Your Ad Spot

Jun 27, 2016

ASILIMIA 87 YA WATANZANIA WANATUMIA POMBE ZA KIENYEJI. MIKOA YA DAR NA MOSHI YADAIWA KUONGOZA

Utafiti uliofanywa unaonesha kuwa, asilimia 87 ya Watanzania wanakunywa pombe za kienyeji huku miji ya Dar es Salaam na Moshi ikitajwa kwamba, inaongoza kwa kuwa na watumiaji wengi wa pombe hizo.

Hayo yameelezwa na Dakta Kissah Mwambene Katibu wa Chama cha Wataalamu wa Afya ya Akili Tanzania wakati alipokuwa akitoa mada kwa Wabunge juu ya madhara na athari za matumizi ya pombe na kuongeza kuwa, takwimu hizo zinatokana na utafiti uliofanywa nchini na Shirika la Afya Duniani (WHO) mwaka 2010. Kwa mujibu wa utafiti, miji ya Dar es Salaam na Moshi inaongoza nchini Tanzania kwa kuwa na idadi kubwa ya watu wanaotumia pombe za kienyeji. 

Dakta Mwambene amesema kuwa, utafiti huo unaonyesha juu ya kuweko ongezeko kubwa la utumiaji wa pombe kupita kiasi nchini Tanzania jambo ambalo limepelekea kuongezeka kwa vitendo vya ukatili wa kijinsia katika jamii. 

Awali akifungua semina hiyo, Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dakta Hamisi Kigwangala alisema kuwa, ulevi ni tatizo kubwa katika jamii na kwamba, asilimia 30 ya vijana wenye umri wa chini ya miaka 15 wameanza ulevi, asilimia 80 ya wasomi wanatumia pombe huku asilimia 63 ya watu wanaokaa maeneo ya jirani na vilabu vya pombe wakitumia ulevi.

1 comment:

  1. Wakati Tanzania ikiongoza kwa kuwa na idadi kubwa ya mitambo ya kutengeneza pombe, idadi kubwa ya walevi, utitiri wa maduka ya pombe na utitiri wa vilabu vya Pombe, Israel inaongoza kwa kuwa na utitiri wa maduka ya vitabu, mitambo ya uchapishaji na maktaba. Hivyo wakati tanzania ikiwatopea kwa umasikini kutokana na nguvu kazi yake kugubikwa na "ulevi Mbwa", wenzetu wanasonga mbele kimaendeleo kutokana na nguvu kazi yake kuzamia kwenye misitu ya vitabu na kujenga utamaduni wa "Elimu Kwanza, badala ya "Pombe kwanza". Lini tutafika walipo wenzetu? Wakati utatupa majibu.

    ReplyDelete

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages