Baadhi ya madaktari bingwa wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, (MNH),
wakipiga makofi wakati wa mkutano wao na Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali hiyo,
Profesa Museru kwenye ukumbi wa CPL wa Hospitali hiyo jijini, Dar es Salaam
Juni 22, 2016.
(PICHA ZOTE NA JOHN STEPHEN WA MNH).
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH),
Profesa Lawrence Museru akizungumza kwenye mkutano huo
NA NEEMA MWANGOMO, MNH
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH),
Profesa Lawrence Museru amekutana na Madaktari wa MNH ikiwa
ni mkakati wa kukutana na watumishi kwa lengo la kuwasikiliza na kujibu kero
zao.
Katika mkutano huo uliofanyika kwenye ukumbi wa CPL uliopo ndani
ya Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Profesa Museru amewapongeza madaktari
hao kwa kufanya kazi kwa bidii na kuimarisha utoaji huduma kwa wagonjwa na
kwamba hali hiyo imechangia MNH kuongeza mapato yake.
Amesema kuongezeka kwa mapato ya Hospitali na kufikia
Sh. bilioni 4. 5 kwa mwezi kumetokana na kila mmoja kutimiza wajibu wake.
Amesema kutokana na mafanikio hayo, MNH imewaongezea
madaktari wake posho mbalimbali ili kuongeza tija katika
utendaji, lakini pia hospitali imeamua kutenga Shilingi Milioni
800 kwa mwaka ili kuwapa mkono wa heri wastaafu wake jambo ambalo
awali halikuwapo.
Hata hivyo amesema mbali na hatua hiyo, pia MNH imefanikiwa
kulipa malimbikizo mbalimbali ya stahiki za wafanyakazi wake
ikiwamo pesa za likizo kwa madaktari pamoja na watumishi wengine kwa
ujumla.
“ Awali changamoto kubwa ilikuwa ni ucheleweshaji wa stahiki za
wafanyakazi kwa Madaktari na watumishi wengine, lakini katika hilo tumefanikiwa
kwani tunaenda nalo vizuri na tumelipa malimbikizo hayo “ amesema Profesa
Museru.
Akielezea mipango ya MNH Profesa Museru amesema
Hospitali ya Taifa Muhimbili ina mipango mbalimbali ya kuendelea kuboresha
huduma zake ikiwemo kuongeza vitanda vya Chumba ya wagonjwa Mahututi-ICU-,
kuongeza ICU ya watoto pamoja na kina Mama wajawazito.
Kaimu Mkurugenzi huyo Mtendaji wa MNH leo Juni 23, 2016
atakutana na Wauguzi pamoja na Maafisa Ustawi wa Jamii.
Baadhi ya madaktari bingwa wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, (MNH),
wakipiga makofi wakati wa mkutano
Baadhi ya madaktari bingwa wakimsikiliza Profesa Museru wakati wa
mkutano huo
Dk Saidia Primos wa hospitali hiyo akiuliza swali kwenye mkutano
huo.
Mkurugenzi wa Fedha, Gerald Kimambo (kushoto) akiteta jambo na
Mkurugenzi wa Upasuaji, Dk John Kimario kwenye mkutano huo
Dk Moa akiuliza swali baada ya kupewa nafasi kwenye mkutano huo
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269