NA K-VIS MEDIA NA
MASHIRIKA YA HABARI
Mgombea kiti cha Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo
(DRC), kutoka upinzani, Moise Katumbi, (pichani) amehukumiwa kifungo cha miaka mitatu
jela Juni 22, 2016 kwa kosa la kumiliki nyumba isivyo halali,
Mwanasheria wake amesema.
Sambamba na kifungo hicho, Katumbi ambaye ni tajiri mkubwa
huko DRC akimiliki klabu maarufu ya soka ya TP-Mazembe, atatakiwa kulipa faini
ya Dola za Kimarekani Milioni 1.
Hata hivyo Katumbi, amehukumiwa huku akiwa ng’ambo
akipatiwa matibabu.
Katumbi amekanusha mashtaka hayo pamoja nay ale ya
kuajiri mamluki kwa nia ya kuuyumbisha utawala kuwa yana msukumo wa kisiasa na
yanalenga kumzuia kuwania nafasi hiyo ya urais.
Wakili wake Barthelemy Mumba Gama ameliambia shirika la
habari la Uingereza, Reuters kuwa hukumu hiyo ni ukiukwaji mkubwa wa sheria
kwani amehukumiwa huku akiwa nje kwa matibabu tena kwa ruhusa ya mwendesha mashtaka
mkuu wa serikali.
Katumbi, ambaye yuko Ulaya kwa matibabu, ndiye mgombea
maarufu zaidi anayetarajiwa kuleta upinzani mkubwa kwa Rais wa sasa, Joseph
Kabila katika uchaguzi unaotarajiwa kufanyika Novemba mwaka huu 2016.
Rais Joseph Kabila
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269