(PICHA ZOTE NA EXAUD MTEI MSAKA
HABARI)
NA EXAUD MTEI
Serikali ya Tanzania imetakiwa kufanya marekebisho
makubwa ya sheria ya mirathi ya kimila sheria ambayo imetajwa kuwa ni kandamizi
na inawanyima haki wanawake na wasichana ikiwa ni utekelezaji wa mkataba wa
CEDAW ambao nchi imesaini mwaka 1986 ambapo ulikuwa unawaelekeza wanachama
kuondoa ubaguzi dhidi ya wanawake katika ngazi za kisiasa,kiuchumi,na kijamii
ili kuletwa usawa.
Wito huo umetolewa leo jijini Dar es salaam na
kikosi kazi cha kamati ya mkataba wa kuondoa aina zote za ubaguzi dhidi ya
wanawake CEDAW ambacho kinaundwa na mashirika tisa yanayotetea haki za wanawake
Tanzania kwa namna mbalimbali.
Akizungumza kwa niaba ya mashirika hayo yote
mkurugenzi mtendaji wa kituo cha msaada wa kisheria kwa wanawake WLAC ambao
wameyaongoza mashirika hayo katika tamko hilo Bi Theodosia Nuhulo ameeleza kuwa
mnamo mwaka 2005 WLAC kwa kushirikana na wadau wengine watetezi wa haki
za wanawake walifungua kesi mkakati katika mahakama kuu ya Tanzania kanda ya
Dar es salaam kupinga vipengele kandamizi katika sheria hiyo ya mirathi (Tamko
la Mirathi la kimila) la mwaka 1963 lakini mnamo mwaka 2006 ilitupilia mbali
kesi hiyo huku ikitamka wazi kuwa vifungu vilivyolalamikiwa ni vya kibaguzi
kweli lakini haiwezi kufanya mabadiliko ya kimila katika tamko la kisheria.
kwa kushirikiana na wadau mbalimbali walifanya jitihada zote za kukata
Rufaa dhidi ya uamuzi huo lakini mnamo 2010 rufaa hiyo ilitupiliwa mbali tena
kwa kigezo kwamba uamuzi na amri iliyotolewa na mahakama kuu ilikuwa na tarehe
mbili Tofauti yani tarehe 8/9/2006 na tarehe 7/12/2006.
Amesema kuwa baada ya jitihada zote hizo kugonga
mwamba juu ya sheria hiyo kandamizi ameeleza kuwa serikali ya Tanzania
kuzingatia ukubwa wa swala hilo kufanya marekebisho ya haraka kwani ndio chanzo
kikubwa cha wanawake wajane nchini Tanzania kushindwa kupata haki zao za msingi
zikiwemo za mirathi baada ya vifo vya wenzi wao
|
Theodosia ameendelea
kusema kuwa pamoja na jitihada nyingi mbalimbali zinazofanywa na WLAC na wadau
mbalimbali watetezi wa haki za wanawake bado serikali haijaonyesha jitihada za
maksudi za kutekeleza Taarifa /maamuzi ya kamati ya mkataba wa CEDAW kuhusu
sheria ya miradhi ya kimila na hali ya wajane Tanzania ili kuhakikisha kwamba
wajane wanapata haki zao.
Aidha WLAC wameitaka serikali ya Tanzania kuwajengea
uwezo majaji na waendesha mastaka na watumishi wa mahakama na wanasheria kuhusu
mkataba wa CEDAW na umuhimu kwa kuzingatia haki za binadam
|
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269