.

MAGAIDI WA ISIS WAUA WATU 20 KATIKA HARAM YA BIBI ZAINAB SA, SYRIA

Jun 11, 2016

Magaidi wa kundi la ISIS au Daesh wametekeleza hujuma ya bomu na kuua watu 20 karibu na Haram ya Bibi Zainab SA katika viungo vya mji mkuu wa Syria, Damascus.
Taarifa zinasema gaidi alijilipua katika lango kuu la Haram hiyo ya Bibi Zainab SA, mjukuu wa Mtume Muhammad SAW.
Mlipuko huo ulifuatiwa na mlipuko mwingine ndani ya gari lililokuwa limetegwa bomu katika mtaa ulioko karibu wa al-Tin.
Magaidi wa ISIS wameilenga Haram hiyo takatifu mara tatu mwaka huu ambapo idadi kubwa ya watu wameuawa na wengine kujeruhiwa.
Syria ilitumbukia katika machafuko ya ndani Machi mwaka 2011 na Umoja wa Mataifa unasema tangu wakati huo watu zaidi ya 400,000 wameuawa. Serikali ya Syria inazilaumu baadhi ya nchi za Magharibi hasa Marekani na waitifaki wake katika eneo yaani Saudi Arabia, Qatar, Uturuki na utawala haramu wa Israel kuwa ndio waungaji mkono wa magaidi wanaotaka kuiangusha serikali ya Rais Bashr al-Assad.

0 Comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

ยช