Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imeandaa vikao 400 maalumu vya usomaji Qur'ani kote nchini
katika mwezi huu Mtukufu wa Ramadhani.
Hayo yamedokezwa na Sayyid Mustafa Husseini, Mkuu wa Masuala ya
Qur'ani katika Shirika la Awqaf ambaye ameongeza kuwa, vikao hivyo
vitahudhuriwa na maqarii sita wa kimataifa kutoka Misri pamoja na
maqarii mashuhuri wa kimataifa Wairani.
Sayyid Mustafa Husseini ameongeza kuwa, taasisi za kielimu,
kiutamaduni na kisayansi zinahusika katika mahafali na jalsa za
kuimarisha ukuruba na mapenzi na Qur'ani Tukufu.
Kwa mujibu wa ratiba, mwaka huu sawa na miaka iliyopita, kutakuwa pia
na vikao vya qasida katika mahafali hizo za usomaji Qur'ani Tukufu.
Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inalipatia umuhimu mkubwa suala la
kuimarisha utamaduni wa Qur'ani kupitia kuandaa programu mbali mbali
kama vile maonyesho ya kimataifa ya Qur'ani ambayo hufanyika kila mwaka
mjini Tehran katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani na mashindano ya
Kimataifa ya Qur'ani ambayo hufanyika kila mwaka mwezi wa Rajab. Aidha
kitaifa hufanyika harakati mbali mbali zinazohusiana na Qur'ani Tukufu.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269