Shaibu Amodu
Siku
chache baada ya kifo cha aliyewahi kuwa kocha wa timu ya Taiga ya
Nigeria, Stephen Keshi, kocha mwingine wa timu hiyo maarufu kama Super
Eagles, Shaibu Amodu naye amefariki dunia, leo akiwa na umri wa miaka
58.
Amodu
aliyezaliwa Aprili 1958, amefariki akiwa nchini Benini, siku tatu tu
baada ya lifo cha Keshi ambaye pia alifia nchini humo.
Stephen Keshi
Wakati
Keshi alidaiwa kuwa na maumivu makali ya kichwa, Shaibu amefariki dunia
baada ya kulalamika kuwa na maumivu makali ya kifua. Inaelezwa baada ya
kudai kifua kuzidi kuuma, aliamua kwenda kupumzika na hakuamka tena.
Amodu pia amewahi kuifundisha klabu kongwe ya Afrika Kusini ya Orlando
Pirates.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269