.

WAZIRI MKUU MAJALIWA AONGOZA MATEMBEZI YA HISANI YA MIAKA 50 YA BENKI KUU YA TANZANIA DAR ES SALAAM

Jun 11, 2016

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza  baada ya kuongoza  matembezi hisani ya kuchangia madawati ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 50 ya Benki kuu ya Tanzania. Matembezi hayo yalianzia Benki Kuu hadi viwanaj vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam. ( (PICHA ZOTE NA KHAMISI MUSSA)
  Gavana wa Benki Kuu, Benno Ndulu, akizungumza kabla ya kumkaribisha mfano wa hundi Waziri Mkuu,  Kassim Majaliwa
 Waziri Mkuu,  Kassim Majaliwa, akitia saini kitabu cha wageni kabla ya kuanza matembezi hayo yalioanzia Benki Kuu
    Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiongoza matembezi ya hisani  ya kuchangia madawati ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 50 ya Benki kuu ya Tanzania. Matembezi hayo yalianzia Benki Kuu nasherehe ya Maadhimisho hayo kuishia  viwanaj vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam Kulia ni Gavana wa Benki Kuu, Benno Ndulu na kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda. Zaidi ya shilingi milioni 262 zilichangwa.

 Waziri Mkuu,  Kassim Majaliwa katika Picha ya pamoja na viong0zi kutoka sehemu mbalimbali wa Benki kuu
Waziri Mkuu KasimMajaliwa (kulia), akikabidhiwa mfano wa hundi yenye dhamani ya Zaidi ya shilingi milioni 262   na Gavana. Benno Ndulu wakati wa Maadhimisho ya matembezi ya hisani ya Miaka 50 ya Benki Kuu ya Tanzania Dar es Salaam, wa katikati ni Mkurugenzi wa Fedha Jamuhuri Ngelime

  Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda akiteta jambo na Waziri Mkuu


 Kikundi cha Sanaa za Maonyesho Jeshi la Polisi Tanzania kikitoa burudani wakati wa Maadhimisho hayo

 Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda akimshukuru Gavana wa Benki Kuu, Benno Ndulu mara baada ya Maadhimisho hayo

 Waziri Mkuu KasimMajaliwa kulia akionyeshwa Noti mbalimbali  za Tanzania na na zanchi nyingine wakati wa Maadhimisho hayo

0 Comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

ª