Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (wa pili kushoto)
akimuuliza jambo Kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza, Ahmed Msangi (kushoto) wakati
walipokuwa wanawasili msikiti wa Rahmani mkoani humo uliovamiwa na majambazi na
kuua waumini watatu ndani ya msikini huo. (Picha
na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi).
Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (aliyevaa Kaunda suti)
akiwa na Kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza, Ahmed Msangi (wa tatu kushoto)
pamoja na askari wengine wa jeshi hilo, wakiyaangalia mapango ya utemini,
jijini Mwanza ambako kulifanyika operesheni ya kupambana na majambazi baada ya
majambazi hao kufanya mauaji katika msikiti wa Rahmani uliopo Kata ya Mkolani
jijini humo
Mzee
wa Msikiti wa Rahmani uliopo Mkolani, jijini Mwanza, Abeid Gati (kushoto),
akimpa fedha mke wa mmoja wa watu waliouawa na majambazi ndani ya msikiti huo.
Fedha hizo zilitolewa na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad
Masauni (aliyevaa Kaunda suti) ikiwa ni rambirambi yake kwa wafiwa wote watatu ambao
walipoteza wenza wao katika mauaji hayo. Hata hivyo Naibu Waziri alisema Serikali
imesikitishwa na tukio hilo la kikatili na pia jeshi lake lipo makini na
linaendelea kulinda usalama wa wananchi na mali zao
Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (aliyevaa Kaunda suti)
akitoka kukagua nyumba za makazi ya askari Polisi zilizopo katika Kambi ya
Mabatini jijini Mwanza, nyumba hizo zimetengewa fedha kwa ajili ya kumaliza
ujenzi katika mwaka ujao wa fedha. Kulia ni Mkuu wa Jeshi la Polisi mkoani
Mwanza, Ahmed Msangi
Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto) akimpa pole
askari Polisi, Mageni Kaseha aliyepigwa risasi ya mguu na majambazi wakati wa
mapambano kati ya polisi na majamabazi hao katika mapango ya utemini, jijini
Mwanza. Askari huyo amelazwa katika Zahanati ya Jeshi hilo iliyopo katika Kambi
ya Mabatini, jijini humo
Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto) akizungumza
na askari polisi katika Kambi ya Mabatini jijini Mwanza, ambao walipambana na
majambazi na kufanikiwa kuwakamata wakati wa operesheni hiyo. Majambazi hayo
yalijificha katika mapango ya Utemini jijini humo na ndipo yakavamiwa na polisi
mara baada ya kuvamia msikiti wa Rahmani uliopo Mkolani jijini humo na kufanya
mauaji. Masauni aliwapongeza askari hao kwa kupambana na majambazi hayo na
kuwasisitiza kuwa kazi bado inaendelea wazidi kupambana mchana usiku ili
wananchi waweze kuishi kwa amani
Mkuu
wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella kimpa taarifa ya hali ya usalama mkoani humo, Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (wa tatu kulia) wakati
kiongozi huyo wa Wizara alipofanya ziara mkoani humo. Katika ziara yake,
Masauni alitembelea mapango ya Utemini mkoani humo ambapo mapambano kati ya
polisi na majambazi yalifanyika, pia alienda kuuona msikiti wa Rahman uliovamiwa
na majambazi, pia alizungumza na wafiwa na baadaye akamaliza ziara yake kwa kuzungumza
na askari polisi ambapo aliwapa pongezi kwa kazi nzuri ya kupambana na
majambazi hao
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269