
Waziri wa
Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (kushoto) akiongoza kikao
kilichoshirikisha watendaji kutoka kampuni zinazojishughulisha na
utafutaji na uchimbaji wa mafuta na gesi za Statoil na ExxonMobil pamoja
na Wizara ya Nishati na Madini na Shirika la Maendeleo ya Petroli
Nchini (TPDC)

Meneja
Mkazi wa Kampuni inayojishughulisha na shughuli za utafutaji na
uchimbaji wa gesi na mafuta ya Statoil Tanzania, Øystein Michelsen,
(kushoto) akielezea shughuli zakampuni hiyo kwa Waziri wa Nishati na
Madini Profesa Sospeter Muhongo (kulia)

Meneja
Mkazi wa Kampuni inayojishughulisha na shughuli za utafutaji na
uchimbaji wa gesi na mafuta ya Statoil Tanzania, Øystein Michelsen
akisisitiza jambo katika kikao hicho.

Waziri wa
Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (mbele) akiongoza kikao
kilichoshirikisha watendaji kutoka kampuni zinazojishughulisha na
utafutaji na uchimbaji wa mafuta na gesi za British Gas (BG), Ophir,
Pavilion pamoja na Wizara ya Nishati na Madini na Shirika la
Maendeleo ya Petroli Nchini (TPDC)
Na Greyson Mwase, Dar es Salaam
Waziri wa
Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo amesema kuwa ili
Tanzania iweze kuwa nchi ya viwanda, nishati ya uhakika inahitajika
na kutaka makampuni kuwekeza katika uzalishaji wa umeme unaotokana na
gesi.
Profesa
Muhongo aliyasema hayo jijini Dar es Salaam katika nyakati tofauti
alipokutana na watendaji wa kampuni zinazojishughulisha na Utafutaji
na Uchimbaji wa Mafuta na Gesi pamoja na wataalam kutoka Wizara ya
Nishati na Madini na Shirika la Maendeleo ya Petroli Nchini (TPDC)
lengo likiwa ni kupokea taarifa ya maendeleo ya miradi mbalimbali ya
makampuni hayo.
Kampuni
hizo zinazofanya kazi kwa kushirikiana na Shirika la TPDC ni pamoja
na British Gas (BG), Ophir, ExxonMobil na Statoil.
Profesa
Muhongo alisema kuwa hakuna nchi yoyote duniani iliyopiga hatua
kimaendeleo bila kuwa na nishati ya uhakika ya umeme na kuwataka
wawekezaji kuchangamkia fursa kupitia gesi nyingi iliyogunduliwa.
Alitaja
maeneo yanayohitaji uwekezaji katika kuzalisha umeme kwa kutumia
gesi kuwa ni pamoja na Mtwara, Lindi, Somanga Fungu, na Mkuranga
Aliongeza
kuwa viwanda 37 pamoja na vya sementi vinahitaji gesi na
kusisitiza kuwa iwapo sekta ya gesi itatumiwa ipasavyo inaweza
kuchangia nchi kupiga hatua na kuingia katika kundi la nchi zenye
kipato cha kati ifikapo mwaka 2025 kama Dira ya Maendeleo ya Taifa
inavyosema.
Wakati
huo huo Profesa Muhongo, aliwataka watendaji kutoka Wizara ya Nishati
na Madini na Taasisi zake kufanya kazi kwa kasi ili kuendana na kasi
ya uwekezaji katika shughuli za utafutaji na uchimbaji wa gesi na
mafuta.
“Sekta ya gesi na mafuta ambayo ni mpya inahitaji umakini na kasi ili kuvutia wawekezaji zaidi,” alisisitiza Profesa Muhongo.
Akizungumzia
mikakati ya serikali katika kuzalisha wataalam katika masuala ya
mafuta na gesi Profesa Muhongo alisema kuwa serikali imekuwa ikitoa
ufadhili kwa wanafunzi katika ngazi za shahada za uzamili na uzamivu
katika vyuo vilivyopo nje ya nchi vyenye uzoefu katika fani hiyo,
pamoja na uanzishwaji wa programu hizo katika Chuo Kikuu cha Dar es
Salaam (UDSM), Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) na Chuo cha Madini.
Alisema
kuwa mpaka sasa kuna idadi ya takribani wanafunzi 98 waliohitimu masomo
hayo na kuziomba kampuni hizo kuajiri wataalam hao ili wawe na
mchango mkubwa kwenye sekta ya gesi.
“ Nia ya
Serikali ni kuwa na wataalam wazawa ambao watanufaika kupitia uchumi
wa gesi kwa kufanya kazi katika viwanda vya kuchakata gesi na
kuzalisha umeme unaotokana na gesi,” alisema Profesa Muhongo.
Naye
Mkurugenzi Mtendaji kutoka Shirika la Maendeleo ya Petroli Nchini (TPDC)
Dk. James Mataragio alisema kuwa shirika hilo limekuwa
likishirikiana na kampuni hizo katika hatua zote muhimu hususan katika
kiwanda cha kuchakata gesi asilia kimiminika (Liquefied Natural Gas)
na kuongeza kuwa mpaka sasa eneo kwa ajili ya ujenzi wa kiwanda
limeshapatikana.
Alisema
kuwa, Tanzania inatarajia kuwa kitovu kikuu cha gesi barani Afrika
kwani gesi nyingi itakayozalishwa itauzwa katika nchi nyingine.
Aliongeza
kuwa nchi kama Uganda, Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo na Zambia
zimeonesha nia ya kuhitaji gesi kwa ajili ya kuzalisha nishati ya
uhakika kwa kuwa nchi hizo zinatumia maji kuzalisha umeme ambapo
uzalishaji wake hupungua hususan wakati wa kiangazi kutokana na
kupungua kwa kina cha maji.
Naye
Meneja Mkazi wa Kampuni ya Statoil Tanzania, Øystein Michelsen,
alisema kuwa kampuni yake ipo tayari kushirikiana na Serikali
kuhakikisha kuwa miradi yake inakamilika kwa wakati.
Alisema
tangu kampuni hiyo kuanza shughuli zake nchini, imekuwa ikishirikiana
na Serikali kwa kutoa ufadhili wa masomo katika masuala ya gesi na
mafuta nje ya nchi kwa wanafunzi wanaofanya vizuri.
Aliongeza
kuwa kampuni ya Statoil imekuwa ikitoa elimu ya ujasiriliamali kwa
wakazi wa mkoa wa Mtwara ili waweze kushiriki katika uchumi wa gesi
kupitia utoaji wa huduma zake kwa Kampuni hiyo.(P.T)
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269