
Mohammed Kuno
Maafisa
nchini Somalia wanasema kuwa mtu anayeaminika kupanga mashambulio ya
chuo kikuu cha Garissa miaka miwili iliopita ameuawa.
Mohamed Kuno aliuawa pamoja na watu wengine wanne na maafisa wa usalama Kusini mwa Somalia.
Serikali
ya Kenya inasema kuwa Kuno ndiye aliyepanga mauaji ya chuo kikuu cha
Garissa ambapo takriban watu 148 na wapiganaji kutoka kwa kundi la
wapiganaji kutoka Somalia al-Shabab.

Garissa
Kuno,ambaye
ni raia wa Kenya alielekea Somalia na pia alilaumiwa kwa mashambulio
kadhaa ya kikosi cha wanajeshi wa Kenya wanaokabiliana na al-Shabab.
Serikali ya Kenya ilitoa zawadi ya zaidi ya dola 200,000 kwa mtu atakayemkamata kufuatia shambulio hilo la Garissa.BBC
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269