
Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa pamoja na Mkuu wa Chuo
Kikuu cha Dar es Salaam Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Makamu wa Chuo hicho
Profesa Rwekaza Mukandala, Balozi wa China hapa nchini lu you Qing, maafisa wa
kampuni ya Kutoka China ya Jiangsu Jiangdu wakiweka mchanga kama ishara ya
kuweka jiwe la msingi katika Maktaba Mpya ya Chuo kikuu cha Dar es Salaam UD
mara baada ya kuwasili chuoni hapo. Maktaba hiyo itakuwa na uwezo wa kuchukua
wanafunzi zaidi ya 2000 kwa wakati mmoja.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.
John Pombe Magufuli akisaini katika Kitabu maalum cha Kampuni ya Jiangsu
Jiangdu construction group inayojenga Maktaba Mpya ya Chuo kikuu cha Dar es
Salaam UD mara baada ya kuwasili chuoni hapo

Mkuu wa Chuo
Kikuu cha Dar es Salaam Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli machapisho ya tafiti mbalimbali
za madini na mambo mbalimbali ya kimaendeleo zilizofanywa na wahadhiri wa chuo
hicho mara baada ya kuwahutubia.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.
John Pombe Magufuli akionesha machapisho hayo

Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja
na Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Dkt. Jakaya Kikwete, Makamu wa Chuo
hicho Profesa Rwekaza Mukandala, Balozi wa China hapa nchini lu you Qing,
Waziri Mkuu mstaafu Jaji Joseph Sinde Warioba na makamu wa Rais katika serikali
ya awamu ya nne Mohamed Gharib Bilal, Waziri wa Elimu Profesa Joyce Ndalichako
na Spika Mstaafu Pius Msekwa mara baada ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa
Maktaba hiyo ya kisasa.

Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Balozi wa
China hapa nchini lu youQing kabla ya kwenda kuzungumza na jamii ya wanachuo kikuu cha Dar es Salaam.

Makamu Mkuu wa
Chuo kikuu cha Dar es Salaam Profesa Rwekaza Mukandala, (kulia), akitoa maelezo kwa Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kuhusu ujenzi wa Maktaba hiyo ya kisasa
itakayochukua wanafunzi zaidi ya 2000 kwa wakati mmoja. Wengine katika picha ni
Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Dkt. Jakaya Kikwete pamoja na Wziri wa
Elimu Profesa Joyce Ndalichako

Makamu Mkuu wa
Chuo kikuu cha Dar es Salaam Profesa Rwekaza Mukandala akitoa maelezo kwa Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kuhusu ujenzi wa Maktaba hiyo ya kisasa
itakayochukua wanafunzi zaidi ya 2000 kwa wakati mmoja. Wengine katika picha ni
Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Dkt. Jakaya Kikwete pamoja na Wziri wa
Elimu Profesa Joyce Ndalichako

Rais
wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, Mkuu wa Chuo Kikuu Cha
Dar es Salaam, Dkt. Jakaya Kikwete, na Waziri wa Elimu, Profesa Joyce
Ndalichako, wakipita kwenye mabango ya picha za mfano wa
majengo ya Maktaba mpya itakayojengwa katika Chuo kikuu cha Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwahutubia mamia ya jamii
ya wanachuo na wananchi mara baada ya
kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa Maktaba mpya itakayochukua zaidi ya
wanafunzi 2000 kwa wakati mmoja.

Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwahutubia mamia ya jamii
ya wanachuo na wananchi mara baada ya
kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa Maktaba mpya itakayochukua zaidi ya
wanafunzi 2000 kwa wakati mmoja.

Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiaagana na baadhi ya Wanafunzi
pamoja na wafanyakazi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam mara baada ya kumaliza
kuwahutubia.

Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiaagana na Waziri Mkuu
mstaafu Jaji Joseph Sinde Warioba mara baada ya kumaliza mkutano huo katika
viwanja vya Chuo Kikuu cha Mlimani jijini Dar es Salaam. (PICHA NA IKULU)
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269