Breaking News

Your Ad Spot

Jun 12, 2016

OLE SENDEKA AWAASA WAMASAI JAMII YA PARAKUYO KUTEUA CHIFU MPYA MWENYE HEKIMA NA BUSARA

Na Bashir Nkoromo, Kibaha
Msemaji Mkuu wa CCM, Christopher Ole Sendeka, ameongoza shughuli ya arobaini ya Kiongozi wa Jamii ya Wamasai wa kundi la Parakuyo, katika Kanda ya mikoa ya Tanga, Pwani, Morogoro, Mbeya na Iringa, Chifu Moreto Ole Maitei, iliyofanyika leo katika Kijiji cha Kigoda, Kata ya Gwata, Kibaha Vijijini katika mkoa wa Pwani.

Katika shughuli hiyo ambayo ilifanyika kimila, Sendeka ambaye alialikwa kuongoza shughuli hiyo Kama kiongozi wa Kimasai anayeheshimika, aliwataka Jamii ya Wamasai Kanada za mikoa hiyo, kuwa na Umoja na kutumia hekima na busara  katika kumpata mrithi wa nafasi iliyoachwa na Chifu Ole Maitei.

Aliwataka kumteua Chifu au Laiboni, mwenye sifa zinazostahili ambazo hata kama Chifu Ole Maitei angekuwepo angerithika kuwa anafaa kuwa mrithi wake.

Kwa heshima aliyopewa katika shughuli  hiyo Ole Sendeka, aliweka kwenye kaburi kibuyu na usinga ambavyo ni vifaa alivyokuwa akitumia Chifu Ole Maitei ambaye ndani ya Jamii hiyo anatambuliwa zaidi kwa cheo cha Laiboni ambaye ni kiongozi mkuu wa viongozi wanaofuatia hadhi yake wanaoitwa Laigwanani. Uwekaji vifaa hivyo ulifayika huku ukishuhudiwa na ndugu jamaa na wanajamii hiyo, Mjane na Dada wa Marehem.

Mmoja wa Malaigwanani waliohudhuria shughuli hiyo, alisema, Kibuyu hicho alichoweka Ole Sedeka kwenye kaburi, ndani kilikuwa na  mawe ambayo Chifu Ole  Maitei alikuwa akiyatumia kubashiri yanayoweza kutokea mbele ya safari huku usinga akiutumia kupungia kuwasalimia wageni au kufukuzia mbali mifarakano na balaa katika jamii yao.

Kabla ya kuweka vifaa hivyo kwenye kaburi, Sendeka alitanguliwa na watoto wote wa kiume kumwaga kwenye kaburi hilo  asali, maziwa ya ng'ombe na mafuta ya kidari cha dume maalum la ng'ombe kama ishara ya kutekeleza mila na desturi.

Chifu  Ole Maitei ambaye alikuwa kiungo muhimu kwa kuunganisha jamii hiyo ya Kimasai  hasa katika utatuzi wa migogoro yawafugaji kutoka jamii hiyo na wakulima katika maeneo mbalimbali ya mikoa ya Tanga, Pwani, Morogoro, Mbeya na Iringa alipokea nafasi ya Uchifu kutoka kwa Laibon Labani Moreto ambaye alifariki miaka ya 2005. PICHA KEM KEM ZA TUKIO HILO>BOFYA HAPA

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages