Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mwenyekiti wa Chama cha UDP mzee John Momose Cheyo mara baada ya kumaliza kuzungumza na wageni mbalimbali katika tukio la upokeaji wa Taarifa ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2015.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo pamoja na Mwanachama wa Chama cha UDP Goodluck Ole Medeye , Mwenyekiti wa UDP, John Cheyo pamoja na Jaji Mark Bomani Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Waziri Mkuu Mstaafu Jaji Joseph Sinde Warioba mara baada ya kuwasili Ikulu kwa ajili ya upokeaji wa Taarifa ya Uchaguzi mkuu wa Mwaka 2015 kutoka Tume ya taifa ya Uchaguzi(NEC)
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania KKKT baba Askofu Dkt. Fredrick Shoo mara baada ya kupokea Taarifa ya Uchaguzi mkuu wa Mwaka 2015 kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi(NEC) Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na mwanasiasa mkongwe John Shibuda huku Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein naye akisalimiana na Mwenyekiti wa Chama cha UDP Mzee John Momose Cheyo mara baada ya kukamilika kwa tukio la upokeaji wa Taarifa ya Uchaguzi mkuu wa Mwaka 2015 kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wakuu wa Serikali,Marais Wastaafu,
Mawaziri Wakuu Wastaafu, Tume ya Uchaguzi na Mabalozi wa nchi mbalimbali mara
baada ya kupokea Taarifa ya Uchaguzi mkuu wa Mwaka 2015 kutoka Tume ya Taifa ya
Uchaguzi (NEC). PICHA ZOTE NA IKULU
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269