.

TAWI LA TUGHE HOSPITALI YA TAIFA MUHIMBILI LAFANYA UCHAGUZI WA VIONGOZI

Jun 10, 2016

 Pichani ni Mwenyekiti Mziwanda Chimwege ambae ametetea nafasi yake kwa kuibuka na kura 248 dhidi ya mpinzani wake Dr. wa watoto Hospitali ya Taifa Muhimbili,  Peter Kibacha kwa kupata kura 46. (PICHA ZOTE  NA KHAMISI MUSSA)
 Mwenyekiti huyo nisiku mbili  baada ya kuibuka mshindi nafasi ya Mwenyekiti wa Tawi la Tughe Hospitali ya Taifa Muhimbili akipitia nyaraka mbalimbali ofisini kwake, ambapo mwenyekiti huyo anawashukuru wanachama wa tawi la  hospitali ya Taifa Muhimbili kwakumpa heshma ya kuwaongoza kwa muda wa miaka mitano ijayo na anawaahidi kuwatumikia kwa busara, hekima, na maarifa yote, na mmoja wa mwanachama ambae hakupenda kutaja jina lake , alisema hakuona haja ya kuchagua viongozi wengine kwa vigezo hao wanafaa na ni wazoefu kwa kufahamu njia zote za kupita na anawaamini niwachapakazi wazuri na kutetea haki za wafanyakazi bila woga

 Katibu, Faustini Kaitaba akiwa ofisini akichapa kazi baada ya siku mbili ambapo amefanikiwa kutetea nafasi yake kwa miaka 5 kwa kura 215 dhidi ya mpinzani wake Peter Bokhe kwa kupata kura 91,
 Wajumbe wakihakiki kura za mwenyekiti
 Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Profesa Lawrence Museru (katikati) akiwa naviongozi wengine wakati wa zoezi la ufunguzi wa Mkutano wa Viongozi wa Tawi la Tughe Hospitali ya Taifa Muhimbili, kushoto ni Mkurugenzi Rasilimali watu, Makwaiya Makani na kulia ni Afisa Utumishi Hospitali ya Taifa Muhimbili, Amos Hangaya
 Baadhi ya wanachama wa Tughe wa Hospiatli ya Taifa Muhimbili wakiwa tayari kuchagua viongozi wapya watakao waongoza kwa kipindi cha miaka mitano ijayo 
 Wajumbe wakiwa katika uchaguzi huo

0 Comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

ª