
UFARANSA ikiwa katika kundi A, la michuano ya EURO2016,
imeanza vema kampeni yake ya kulitwaa kombe hilo baada ya kuibuka mshindi wa
mabao 2-1 dhidi ya Romania katika pambano la ufunguzi la michuano hiyo
lililopigwa kwenye uwanja wa Stade De France, huko Saint Denis nchini Ufaransa
usiku wa kuamkia leo Juni 11, 2016.
Oliver Girou aliipatia timu yake ya Ufaransa bao la
kuongoza, kunako dakika ya 58 kabla ya Bogdan Stancu wa Romania
kusawazisha bao hilo ,unako dakika ya 65. Wakati pambano hilo linaelekea
ukingoni, katika dakika ya 89, Dimiotri Payet wa Ufaransa alifunga bao la pili na hivyo kuondoa
matumaini ya Romania kwenda sare na wenyeji hao wa michuano ya mwaka huu
EURO2016.

Dimiotri Payet(kulia), akishangilia bao na mwenzake

Oliver Girou, akishangilia bao lake la kwanza

Bogdan Stancu, akifunga penati

Kikosi cha Romania
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269