
Gari la polisi likimwaga maji ya
kuwasha, kuwatawanya mashabiki wa soka walioamriwa kurudi nyumbani baada
ya uwanja wa taifa kujaa "pomoni" majira ya saa sita mchana Juni 28,
2016. Yanga inatarajiwa kumenyana na TP-Mazembe ya DCR kwenye michuano
ya kombe la Shirikisho la CAF hatua ya robo fainali. (PICHA NA K-VIS MEDIA/KHALFAN SAID)
NA K-VIS MEDIA
UONGOZI wa uwanja wa taifa jijini Dar es
Salaam, umelazimika kufunga mageti yote ya kuingilia uwanjani humo
baada ya uwanja huo kujaa "pomoni" ilipofika saa 6 mchana.
Polisi walifanya kazi ya ziada kuwazuia
maelfu ya mashabiki wa soka waliojihimu mapema kufika uwanjani, ili
kujionea pambano hilo la soka ambalo Yanga ilitangaza kuwa halitakuwa na
kiingilio.
Polisi walilazimika kutumia mabomu ya
kutoa machozi na maji ya kuwasha ili kuwatawanya mashabiki hao wa soka
ambao licha ya kuwaambia uwanja umejaa na warudi nyumbani ili kuona
pambano hilo kupitia matangazo ya moja kwa moja ya runinga.
Hata hivyo mushawishi huo ulishindikana na hapo ndipo polisi walipoamua kufyatua mabomu na kurusha maji ya kuwasha.
Polisi walipata upinzani kidogo baada ya
baadhi ya mashabiki kuanza kurusha mawe hata hivyo sio kwa muda mrefu
kwani polisi waliongeza jitihada za kuwadhibiti na baada ya masaa mawili
jitihada hizo zilizaa matunda














No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269