Mmoja wa kijana ambaye alifika kushuhudia tukio hilo akipanda juu ya Ghorofa baada ya kunusurika kudondokea katika moto huo
Mbele
ni Gari la zima moto likiwa limefanya juhudi za kuzima moto , hapa
wakiondoka kufuata maji mengine ili kuendelea na zoezi la kuzima moto
huo
Moto ukiendelea kuwaka katika Bohari hilo
Baadhi ya Mashuhuda wakishuhudia tukio hilo la kuwaka kwa Bohari
Magari yakiwa yameruhusiwa kuendelea na safari baada ya moto huo na moshi mkubwa kupungua. Picha na Fredy Njeje/Blogs za mikoa
BOHARI ya kuhifadhi mataili na vifaa vyengine
vya magari lililopo eneo la Sinza Lego limeteketea kwa moto na kusababisha hasara ya mamilioni ya shilingi.
Kwa mujibu wa chanzo chetu kutoka eneo hilo kilidokeza kuwa moto umeteketeza mataili, huku chanzo cha tukio hilo bado hakijafahamika.
Chanzo hicho pia kilisema kuwa mmiliki wa ghala hilo hajakufahamika kwa jina, hivyo jitihada za kumtafuta zinaendelea ili kuzungumzia hasara ya mali iliyoteketea kwa moto.
Alisema jirani ya bohari kulikuwa Gereji ambayo haikuathirika na moto, mpaka jioni kikosi
cha zimamoto kiliendelea kusaidiana na wananchi
kuhakikisha moto huo unazimika.
Hata hivyo juhudi za kumtafuta kamanda wa polisi Mkoa wa Kinondoni zinaendelea kuelezea.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269