Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye ambaye pia ni Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM (NEC), Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye leo ameongoza kuuaga mwili wa Mpigapicha Mkuu wa Tanzania Daina, Joseph Senga (pichani), ambaye ni mpigapicha mkongwe, aliyefariki dunia nchini India alikokuwa akipatiwa matibabu. Mwili wa Josefu Senga uliwasili nchini jana, na kuagwa leo, Sinza jijini Dar es Salaam, kwa ajili ya kusafirishwa kwenda kuzikwa nyumbani kwao mkoani Shinyanga.
Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo Nape Nnauye akitoa heshima kwenye mwili wa marehemu Joseph Senga, Sinza jijini Dar es Salaam, leo
Naibu Wazri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Anastazia wambura akitoa heshima kwa mwili wa Marehemu Joseph Senga leo Sinza Jijini Dar es Salaam
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe ambaye pia ni mmiliki wa Kampuni ya Free Media wachapishaji wa gazeti la Tanzania taima alilokuwa akifanyia kazi Joseph Senga, akitoa heshima mwa mwili wa marahemu Joseph Senga. Wafuatao ni waombolezaji wengine wakitoa heshima kwa mwili wa marehemu Joseph Senga
Mjane wa Marehemu Joseph Senga akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu mumewe
Jeneza lenye mwili wa marehemu Joseph Senga likibebwa kuingizwa kwenye gari tayari kwa safari, waliobeba jeneza hilo wengi wao ni wapigapicha za habari
KABLA YA KUAGA MWILI
Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo Nape Nnauye ambaye pia ni Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi CCM, akiteta jambo na Waziri Mkuu wa zamani, Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, Edward Lowassa kabla ya hatua ya kuaga mwili wa marehemu Joseph Senga. Kulia ni Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe
Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo Nape Nnauye ambaye pia ni Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi CCM, akiteta jambo na Mwenyekiti wa Chadema Joseph Senga Freeman Mbowe, kabla ya hatua ya kuaga mwili wa marehemu Joseph Senga
Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo Nape Nnauye ambaye pia ni Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi CCM, akisalimiana na Askofu wa kanisa la Kiinjili la Kipentekoste William Mwamalanga, wakati wa shughuli hiyo ya kuaga mwili wa marehemu Joseph Senga. KWA PICHA ZAIDI ZA MSIBA HUU>>>BOFYA HAPA
Your Ad Spot
Jul 31, 2016
Home
Unlabelled
WAZIRI NAPE AONGOZA KUAGA MWILI WA MPIGAPICHA MKONGWE JOSEPH SENGA, JIJINI DAR ES SALAAM, LEO, AKUTANA NA LOWASSA, MBOWE
WAZIRI NAPE AONGOZA KUAGA MWILI WA MPIGAPICHA MKONGWE JOSEPH SENGA, JIJINI DAR ES SALAAM, LEO, AKUTANA NA LOWASSA, MBOWE
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post Top Ad
Your Ad Spot
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269