Na
Mwandishi Maalum, New York
Bodi
ya Ukaguzi ya Umoja wa Mataifa, ambayo
Mwenyekiti wake ni Mkaguzi na
Mdhibiti n Mkuu
wa Hesabu za Serikali, ( CAG)
Profesa Mussa J. Assad jana ( Jumanne) imerejea na kuidhinisha
ripoti kumi na moja za Mashirika, Mifuko na shughuli
mbalimbali za Umoja wa Mataifa.
Katika
kikao hicho cha 70 kilichofanyika hapa
Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa,
pamoja na kuidhinisha ripoti za
Mashirika na Mifuko
iliyochini chini ya Umoja wa
Mataifa, pia Bodi ilipokea taarifa mbalimbali za kiutendaji
zinazohusiana na majukumu ya
Bodi hiyo.
Wajumbe
wa Bodi ya Ukaguzi ya Umoja wa Mataifa, ni Mkaguzi na
Mdhibiti Mkuu wa Hesabu wa Serikali
ya India, Bw. Shashi Kant Sharma, Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu
za Serikali ya Uingereza, Sir Amyas Morse, na Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Prof. Mussa J. Assad.
Pamoja
na kupitia na kuridhia ripoti hizo kumi
na Moja, na kupokea taarifa za kiutendaji, shughuli nyingine
iliyofanywa na Bodi ya Ukaguzi ilikuwa ni pamoja na kuiaga Ofisi ya Ukaguzi ya Uingereza baada ya
kumaliza kipindi chake cha miaka
sita ya uhudumu katika Bodi hiyo.
Hafla
ya kuagwa kwa Ofisi
ya Ukaguzi ya Uingereza ilihudhuriwa
na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa,
Bw. Ban Ki Moon pamoja na wadau mbalimbali ambao ni wateja wa Bodi ya
Ukaguzi ya Umoja wa Mataifa.
Nafasi ya
Ofisi ya Ukaguzi ya Uingereza
imechukuliwa na Ofisi ya Ukaguzi
ya Ujerumani ambayo imekaribishwa rasmi kuwa mjumbe wa Bodi hiyo.
Akizungumza
katika hafla hiyo ya kuiaga ofisi ya Ukaguzi ya Uingereza na
kuikaribisha Ofisi ya Ukaguzi ya
Ujerumani, Mwenyekiti wa Bodi, Prof.
Mussa Assad amemshukuru Sir. Amyas Morse kwa mchango wake yeye binafsi na Ofisi yake
kwa uwajibikaji mkubwa na weledi wa hali
ya juu ambao umefanikisha
utekelezaji wa mamlaka na majukumu ambayo Bodi hiyo imekabidhiwa na
Umoja wa Mataifa.
Akiikaribisha
Ofisi ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Ujerumani, Prof. Assad
ameelezea matumaini yake ya
kufanya kazi kwa karibu na ushirikiano wa hali
ya juu na mjumbe huyo ili kwa pamoja waweze kutekeleza majukumu na
mamlaka waliyokabidhiwa na Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa.
Bodi
ya Ukaguzi ya Umoja wa Mataifa,
ilianzishwa mwaka 1946 na Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kwa lengo
la kukagua hesabu za Mashirika, Mifuko
na Taasisi nyingine zilizo chini ya Umoja wa Mataifa, ili
pamoja na mambo mengine kuhakikisha kwamba Taasisi hizo zinatekeleza
majukumu yake kwa mujibu wa kanuni na taratibu za Umoja wa Mataifa ikiwa ni pamoja na matumizi
yenye tija na adilifu ya bajeti kulingana na
mamlaka ya Mashirika na Taasisi
hizo.
Bodi
ya Ukaguzi inatekeleza majukumu yake
kama chombo huru na taarifa zote za ukaguzi huwasilishwa kwa Baraza Kuu
la Umoja wa Mataifa pamoja na wateja
ambao wanakaguliwa na Bodi
hiyo.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269